Vipaumbele vya taifa letu hupangwa na nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipaumbele vya taifa letu hupangwa na nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AmaniKatoshi, Nov 19, 2010.

 1. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Katika hotuba yake bungeni tarehe 18 november , 2010, Raisi JK aligusia kwa umahiri vipengele 13 vya serekali yake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

  Kwa mujibu wa gazeti la Habarileo la tarehe 19 November, kipengele cha 13 kilikuwa (nanukuu)

  "Kipaumbele cha mwisho ni kulinda mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kukamilisha ahadi za mwaka 2005 ambazo hazijatekelezwa"

  Leo gazeti la Tanzania daiam limetoa TAARIFA ya Tanesco kuhusu mgao mkubwa wa umeme.

  Sasa tukiangalia matatizo ya umeme yaliyoikumba nchi wakati JK anaongoza miaka 5 ya kwanza hadi kufikia Lowassa kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond...tujiulize

  Je mamatizo ya umeme yanahusiana na kipaumbele cha 13?

  Je, kipaumbele cha pili cha kukuza uchumi kinalindwaje na kurudisha mgao wa umeme?

  Je katika listi ya mikoa inayoanza kukaa gizani toka leo (isource: tanzania daima), kuna uhusiano kati ya Mkoa wa Kinondoni, Arusha na Kilimanjaro kukosa umeme kwa sababu walichagua wapinzani?

  Je machungu ya umeme ni moja ya yale yaliyotabiriwa hapa JF kabla ya 31/October?

  Nisaidieni wana Jf
   
 2. oba

  oba JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa miaka kadhaa sasa ya uhuru wa nchi zetu, Tanganyika na Zanzibar, tumeshuhudia kila mtawala akija na vipaumbele vyake juu ya wanachi na nchi kwa ujumla. Mara nyingi tu baada ya mtawala huyo kuondoka madarakani anayemfuatia huja na vipaumbele vyake vingine pengine tofauti kabisa na vya mtangulizi wake. mfano huyu aweza kuuza nyumba za Serikari na mwenzie akataka kuzinyang'anya, mmoja aaweza kubinafsisha mali za serikali na mwenzie akazipokonya.

  Vipaumbele vilivyoweza kudumu kwa muda mrefu katikati ya watawala ni vile vilivyo chini ya sera za kimataifa kama millenium development goals.Nani anapanga vipaumbele nyetu?ili umeme isiwe shida tena, maji , elimu, ajira n.k?

  Kuna haja ya kuwa na Baraza la Senate (if possible katiba mpya ilizingatie hilo!) ambalo kazi yake itakuwa kuona mbali na kuweka malengo na vipaumbele vya taifa. Mfano, baraza hilo laweza kuweka 20 years plan za kuhakikisha tuna umeme wa kutosha, 10 years za kuondokana na ukosefu wa maji salama n.k

  Baada ya kuwekwa vipaumbele hivyo, chama cha siasa kinachotaka kushika dola kitaleta sera za namna gani kitatupeleka kule vipaumbele vyetu vinapotaka, wananchi watazipambanisha mbinu hizo na kuchagua moja za chama fulani na kukipa muda wa kuongoza utekelezaji wake, baada ya miaka mitano wananchi watachanganua ni kwa kiwango gani chama hicho kimeongoza kuelekea malengo yetu, na wataamua kama wakirejeshe madarakani au la.

  Baraza hilo members wake waweza kuwa maraisi wastafu, mawaziri wakuu wastafu au hata majaji wakuu wastafu. Sharti members hao wajiondoe kwenye vyama vyao kabla ya kuwa members wa hilo baraza. Baraza halitakuwa la chama wala mtazamo wa chama chochote bali mtazamo wa taifa.

  Kwa namna hiyo tutaweza kuondoa mtafaruku wa kila chama kuja na vipaumbele vyake visivyotekelezeka kwa nia ya kuwadang'anya wananchi na kushika dola.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hupangwa na wenye nchi, yaani CCM
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwa sasa Tanzania yetu haina vipaumbele. Hakuna kitu tunachofanya kama nchi, kama mikoa na kama wilaya. As people we are doomed, hasa kutokana na waliojuu yetu kutokuwa na nia.

  Ni rahisi kusema hivi kwa kuwa wakati wa Nyerere kulikuwa na lengo, njia na juhudi za kufikia maelngo hayo. Hata Rais alipokuwa anafanya kazi kila siku alikuwa anafanya kazi kuelekea kutekeleza malengo yale.

  Leo ukiuliza rais anafanya nini kila siku kwa lengo lipi, mkuu wa mkoa anafanya nini kila siku kwa lengo lipi, mkuu wa wilaya, au chama tawala kinafanya nini, huwezi kupata majibu. Kinachoitwa vision 2025 ni karatasi tu ambayo ukiangalia toka ilipoandikwa hadi leo hakuna significant kilichofanyika, inayoitwa ilani ya chama pia ni ahadi amabazo hazitekelezeki na ni maneno ya kuombea kura.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na Rostam Aziz, Edward Lowasa, Salma Kikwete, Ridhiwani Kikwete na King Jakaya Kikwete
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Hao ndo strategists wa Tz. Nyuma yao kuna akina Makamba, Pinda, Hiza, Msekwa na Ngeleja
   
 7. Researcher

  Researcher Senior Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii hoja ni ya msingi sana. Kwa ninavyofahamu wizara na idara hupanga na chama tawala huambatanisha mipango hii kwenye ilani yake.

  Hata hivyo chama tawala hufanya mabadiliko kidogo kuongeza mvuto ktk kampeni. Naamini ni vema kuwa na mchango wa watekeleza sera katika uundaji sera.

  Ushiriki wa wananchi na wadau wengine bado ni duni haswa ukizingatia warsha za mipango hufanyika mahotelini kwa gharama kubwa.

  Hata hivyo mfumo wetu wa siasa unawapa fursa baadhi ya mawaziri kupindisha mwelekeo wa mipango hii na kuleta fikra zao.
  Hili ni tatizo kubwa haswa kwa wizara zisizo na ma katibu wakuu thabiti.

  Bila shaka tunahitaji mfumo utakao wabana kusimamia mipango iliyowekwa na si kila uchao kuamka na jipya, na kama kuna ulazima wa mabadiliko basi liwe ni swala shirikishi.

  Swali langu ni Je, vyama vingine huandaa vipi ilani zake?, ni kwa utashi wa viongozi au wanawahusisha wadau mbali mbali wakiwemo watendaji na wananchi?. Nauliza kwa nia nzuri ya kuhakikisha utekelezaji unakuwa halisi.

  Na Je, Ni kwa namna gani tunaweza kufahamu endapo chama tawala kinatoa mwongozo mzuri, au upotoshaji kwa watendaji wa serikali wasio wanasiasa?
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Swali lako ni zuri sana na hata ukiwauliza ccm wanaweza kukujibu ni kwa nini unakiri hizo sera na kuzitekeleza wao wenyewe? Watakwambia kwamba sera hizi zinatunwa na wataaluma wa nchi hii hii ambao wanaielewa na kuelewa nini ni muhimu kwa wananchi.

  Bahati baadhi ya vyama vya siasa ninavyoelewa vimeamua kuwatumia hawa katika utengenezaji wa sera na zinakubalika hata kwa ccm, na bahati mbaya hawa ccm wanawadhalau kwa sababu si wana ccm na angalia mwisho wake ni upi! kiongozi wa serikali kusema hajui umaskani wa mtanzania unatokana na nini.

  Teh teh teh teh teh teh teh
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Leo hii ni takribani siku 20 tangu wabunge wetu watoke majimboni kwao. Katika muda huo zaidi ya shs.2bilioni zimetumika katika kulipa usafiri, posho ya kujikimu na gharama mbali mbali. Hata kazi ambayo wamekuwa wakiifanya katika kipindi hicho haina tija yeyote. Kwa staili hii tutafika?
   
 10. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF,

  Leo nimeona nilete hoja hii ili tuweze kuichangia kwa kufanya uchambuzi yakinifu kufuatia janga la Mabomu yaliyolipuka jijini Dar es Salaam.

  Serikali imesema hakukuwa na upungufu wa madawa wala vitendea kazi. MSD inasemekana walitoa vifaa na madawa kwa hospitali za Amana na Muhimbili kuhakikisha kuwa hakuna upungufu unaojitokeza na kuwa Serikali itagharamia mazishi ya marehemu wa mabomu. Wanaenda mbali zaidi na kuahidi kuwa baada ya tathmini waathirika wa mabomu watalipwa fedha kufuatana na uharibifu utakaokuwa umefanywa.

  Sasa Ni kitu gani huwa kinasababisha vifaa na madawa kutopatikana katika hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati?

  1. kwanini wananchi wanapodai haki au huduma wananchi hao hujibiwa kuwa uwezo ni wa serikali ni mdogo. Sawli moja je wakati wanaposababisha makosa kwa uzembe kama huu wa mabomu (uliotokea mara mbili) fedha hutoka wapi?

  2. Vipaumbele vya taifa wanavipataje?

  3. Kwanini masuala yasiyo na tija kwa wananchi ndiyo yanayopewa vipaumbele kama malipo ya Dowans, wizi katika BoT, Kuwalinda wawekezaji wasio na mitaji, Wauaji wa raia kwa kisingizio cha kulinda wawekazaji kwa kigeni!? masiuala yanayogusa watz wengi hasa elimu haina kipaumbele. Mf. Vyo vikuu, sh. 10,000 inaonekana ni nyingi sana wakati wakuu wanalipwa per Diem ya zaidi ya 100,000. Hawa wanafunzi ndio wataalamu watakaoongoza nchi hii. hivyo ni lazima kuwekaza huko.

  Sasa tatizo hili tunaweza kulimalizaje ili watawala wetu waweze kushughulikia mahitaji ya wananchi badala ya kushughulikia mambo yao yasiyo na tija kwa wananchi?
   
 11. m

  mzambia JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wasaidizi wake wawe wanasoma haya mambo jamvini na wampelekee mkwere na kumshauri labda atabadilika
   
Loading...