Vipaji hivi vya zamani vimetoweka?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
385
Miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na jamaa mmoja mwenye nguvu za ajabu alikuwa anaitwa pawa mabula na baadaye walijitokeza wengine kama pawa masalu,mwanakatwe nk,walikuwa na michezo mizuri sana ya kutumia nguvu kama kuvuta gari kwa meno,kuzuia pikipiki kwa nywele,kupasua mawe kwa kichwa na mingine mingi,je wako wapi siku hizi au wameondoka na vipaji vyao?
 
Kwa sasa Power Mabula ni Mchungaji amefungua kanisa lake la walokole mtaa Wa ole matejo jijini Arusha.sasa anatoa pepo kwa nguvu ya Yesu
 
Kwa sasa Power Mabula ni Mchungaji amefungua kanisa lake la walokole mtaa Wa ole matejo jijini Arusha.sasa anatoa pepo kwa nguvu ya Yesu
sema kweli ndugu yangu,nadhani umri utakuwa umeenda kidogo
 
Kila kitu kinawakati wake sasa ivi ni awamu ya kata K
pia awamu hii itapita na tutaikumbuka
 
Daah! Power Mabula kitambo sana!

Mwenyewe alikua akijisifu kabla ya kuanza michezo yake kwa kusema"Power mabula mtoto wa pekee,sina Kaka sina Dada,nilizaliwa peke yangu!"
 
Dah power mabula. Enzi hizo. Familia yake ilikua pale Mzinga jeshini Morogoro. Huyu alikua balaa sijui walikua wanatuibia kimazingaombwe au kweli. Maana unalala Chini halafu gari inakupitia na unaamka fresh tu? Na unavuta scania kwa kutumia meno? Au ni sayansi flan
 
Kuna sayansi na ulozi. Ni ngumu kutofautisha. Hata mazingaumbwe mashuleni sijui yalipigwa marufuku?
Inafaa mtu huyo akavute mascania yaliyokwama porini ili nimwamini.
 
Back
Top Bottom