Viongozi wetu wanajenga taifa au nchi?

Viongozi wetu wanajenga taifa au nchi?

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,186
Reaction score
5,455
Mnara wa babeli ulivurugwa na MUNGU na kuwa chanzo cha uwepo wa lugha nyingi hadi leo baada ya MUNGU kugundua kuwa walichokifanya wanadamu ilikuwa kumkufuru MUNGU.

Nchi yetu imetapakaa matukio mengi ya ajabu na ya kutisha yanayoashiria wazi kuwa hatuna taifa lililojengwa imara. Taifa imara lina watu wenye upendo, undugu,mshikamano na amani miongoni mwao. Ndani ya taifa imara hakuna magomvi yaliyosababishwa na utofauti wa mitazamo ya watu bali ni faraja tu.

Ni wazi kuwa ukijenga taifa imara ujue kuwa nchi inaweza kujijenga yenyewe. Mfano watu waliungana pamoja bila kujali utofauti wa imani zao na mitazamo wakakaa pamoja wakajenga shule, zahanati na miundombinu mingine mingi. Hii ni kwasababu walikuwa TAIFA moja.

Leo hii mauaji na magomvi ktk nchi yametapakaa kwasababu viongozi wetu wako bize kujenga nchi badala ya kujenga TAIFA la watu wamoja. Ukijenga nchi bila kujenga taifa kwanza ujue nchi itabomoka tena ila ukijenga TAIFA ujue TAIFA litajenga NCHI na haiwezi kubomoka kwa kuwa misingi yake ni imara mno.

Enyi viongozi wa nchi hii jengeni TAIFA la watu wamoja kwani kwa mwenendo wa nchi ulivyo siioni nchi wala TAIFA moja bali nayaona mataifa mengi ktk nchi moja.

Ni wazi kuwa KUUMIZWA MAISHANI NI JAMBO LA KAWAIDA MNO LAKINI KUENDELEA KUVUMILIA KUUMIZWA NI MAAMZI YA MUUMIZWAJI MWENYEWE. Kanuni,sheria,taratibu na miongozo iliyokandamizi kwa nchi inayoendelea kutungwa na kutolewa ktk nchi hii ipo siku itakuwa sururu la kuibomoa nchi hii inayojengwa.
MUNGU ibariki dunia hii na watu wake wote.
 
Dhamira ya Magufuli Ni nzuri ila Kuna watu wachache wasiopenda kuambiwa ukweli Wao ndo wanatuvurugia mambo.lazima wakubali kuwajibika
 
Dhamira ya Magufuli Ni nzuri ila Kuna watu wachache wasiopenda kuambiwa ukweli Wao ndo wanatuvurugia mambo.lazima wakubali kuwajibika
Fafanua vizuri tuelewe hiyo dhamira. Ujue rais siyo mtu wa kulalamika kama raia wengine kwa kuwa ana authority nyingi .
 
Back
Top Bottom