Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutotia saini mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi yaliyopitishwa na wabunge.
Viongozi wetu wasiishie kumpongeza tu pia wawe mstari wa mbele kumshauri mambo muhimu kama haya. Nilitegemea ushauri kama huu kutolewa na viongozi wetu wa dini kwa rais Magufuli kabla ya kusaini muswada wa vyombo vya habari na ule wa sheria ya mitandao inayoonekana kukiuka haki ya binadamu kuwa huru kutoa maoni yake.
Wiki iliyopita wabunge wa upinzani (CORD) walipinga sheria itakayoruhusu kuhesabu kura kwa njia ya kawaida pale ambapo mashine za kuhesabu kura zitakwama au kushindwa kufanya kazi hiyo.
Wametishia kuingia barabarani ifikapo jan 4 iwapo sheria hiyo itasainiwa.
Kenya inajiandaa kufanya uchaguzi wake mkuu August mwaka ujao.