Viongozi wetu na 'title' bandia

Unachotaka kusema nini unaonekana mambo ya hapa duniani hujui kabisa pengine tukusaidie hebu sema unachotaka ni nini hasa?
huu ukali wote sababu unajua tunakuja kumshukia dokta feki jakaya kikwete anayelobby kutunukiwa udaktari...
 

Ubarikiwe mkuu kwa kutokupepesa macho
aondolewe haraka hapo
 
Unachotaka kusema nini unaonekana mambo ya hapa duniani hujui kabisa pengine tukusaidie hebu sema unachotaka ni nini hasa?


Nilivyoelewa mimi anataka kujua, ni kwa nini mtanzania au baadhi ya watanzania wakiwa na elimu kubwa i.e Phd, wanapenda saana kutukuzwa (kusifiwa) na elimu yao...!? nipo tayari kukosolewa ikiwa nimemwelewa vibaya.
 
Tatizo mnashindwa kutofautisha honorary awards na awards za kusotea. Ulaya wanasiasa wengi wenye honorary PhDs wanafuata masharti ya honorary hasa lile la kutolitumia kwenye official addressing. Hapa bongo ni foul tu, mtu ana honorary kama JK, Mengi, Karume etc halafu kila siku wanaitwa ma Dr. hadi kwenye vyombo vya habari. Mtu aliyeusotea uDr. au uProf. wake hata akijiita hadi chooni sioni shida yoyote mie.
 
Swadakta mkuu..Hizo ni academic title, zinafanya kazi tu pale unapokua mazingira ya universities. Sio mtu bungeni ni prof, dr, dah......ulimbukeni wa hali ya juu.
 
Kuna wakina profesa Maji marefu, Nasikia Stella Manyanya ana elimu ya fundi mchundo lakini naye anajiita Injinia Manyanya.

Inabidi tufike wakati tuseme ukweli kuhusu hili,Sijawahi kusikia Nyerere sehemu yoyote akijiita profesa Nyerere japokuwa alikuwa alikuwa profesa,alipenda kuitwa mwalimu. viongozi wa sasa wamejaa sifa na kufikiri akiitwa profesa ama dr basi ataogopwa.
 
Mimi nimemwelewa vizuri ila wewe ndiye huelewi au hutaki kuelewa. Hata Hillary Clinton sijawahi sikia akiitwa Dr Hillary Clinton, au Dr Gordon Brown etc etc. Ukweli ni kwamba vyeo vya kisomi vinatumika tu unapokuwa kwenye mambo ya academic na siyo kwenye siasa au mitaani. Ndiyo maana ukienda UN watu wengi ni ma Phd holders na hutakiwi kutumia hizo title, wengi ni former professors ila huruhusiwi kutumia vyeo vya academic kazi ambayo siyo ya academic.
Kwa hiyo niseme hapa Tanzania ni ulimbukeni ndio unawasumbua na nadhani wenzetu uwa wanatucheka sana. Mfano hata zile degree za heshima za akina Kikwete eti naye anashadadia kuitwa Dr Kikwete!!

Unaonekana hujui kitu sijui usaidiweje mkuu.
 
Hivi ni kwa nini hapa nchini kwetu (TZ) huwa ni muhimu sana au tuna mazoea ya kumuita mtu mwenye PhD, Dr. fulani au Prof. fulani kama vile Dr.Magufuli, Dr.Slaa au Dr.Kikwete, Dr.Lamwai au Prof. Muhongo au sijui Prof.Kapuya au Prof.Magembe n.k?
Mbona nchi nyingine hasa za Wazungu hakuna hayo mambo?
Kwa mfano Raisi wa Marekani Baraka Obama ni prof. lkn sijawahi kusikia hata siku moja Mtu akisema Prof. Obama kwanza wanasiasa wengi sana wa Ulaya na Marekani wana PhD lkn sijawahi kusikia Mtu akiwaita Dr.!

Kwa Wazungu au Nchi za Ulaya na Marekani Mtu ataitwa kwa kutumia Dr. au Prof. pale tu anapokuwa yuko kwenye mambo ya kielimu, kwa mfano Raisi Baraka Obama akienda Chuo kikuu cha Harvard basi watamuita Prof.Obama lkn sio mitaani kama hapa kwetu, utakuta hata mitaani kama mtu ana PhD ukimuita bila ya kuweka hilo Dr. ni ugomvi sasa ni kwa nini?
 
Mrema naye siku hizi anaiwa Dokta Augustine Lyatonga Mrema, msiniulize kasomea wapi, jibu ni sijui.
 

Hii ni aibu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…