Viongozi wasio waadilifu wametuponza - JK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
Geee! Tumechoka na kauli zako zisizo na vitendo kila kukicha! Vunja baraza lako la mawaziri na mafisadi wote na waroho wa kujilimbikizia utajiri kupitia nyadhifa zao uwatose! Na wewe mwenyewe kama siyo safi ni bora ujitose tu! :(

Viongozi wasio waadilifu wametuponza - JK
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,February 04, 2008 @00:02

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amesema imani ya wananchi kwa viongozi inaanza kupungua kutokana na ukosefu wa uadilifu na uaminifu, hali ambayo inahitaji kushughulikiwa haraka kabla hali haijawa mbaya.

Kikwete alionya jana Chake Chake, Pemba, kuwa suala la kutokuwa waadilifu linasumbua na kuudhi wananchi, hali inayowafanya wawe na chuki, kukosa imani na hata kuwapotezea heshima viongozi pamoja na chama.

Akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya miaka 31 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uwanja wa Gombani, alitahadharisha kuwa upo uwezekano wa kiongozi kufanya mambo mengi mazuri, lakini iwapo uadilifu wake hauridhishi, ataendelea kukataliwa na wananchi.

Akikumbushia uamuzi alioutangaza hivi karibuni wa kuwadhibiti viongozi wa kisiasa wanapokuwa madarakani kutokujishughulisha moja kwa moja na biashara, Rais Kikwete alisema hilo ni miongoni mwa mambo yanayopunguza imani. “Imani ya viongozi na wananchi inaanza kupungua.

Na inawezekana yanayotufanya tupunguze imani ni mambo haya. Na mtaji wetu viongozi ni wananchi kuwa na imani na sisi. Siku wakipoteza imani na sisi, mjue tumekwisha. Na uhai wetu unatoweka. Tunataka tuendelee kuaminiwa na kupewa ridhaa,” alisisitiza.

Aliendelea kuonya, “Haya tusipoyafanya, tutafanya mambo mengi mazuri, ya barabara, ya maji, ya umeme, ya kuwapa maziwa na asali, lakini ukienda pale ukaona bado wanakataa, kumbe kinachowaudhi sasa wanajadili uadilifu wako, wanajadili uaminifu wako.” Alisema sheria ya kuzuia mawaziri na wabunge kufanya biashara itakapopitishwa, hakuna haja ya wanasiasa hao kuwakabidhi watoto wao mali kwa kificho, bali wanatakiwa kutamka wazi, ili mali hizo zikabidhiwe kwenye dhamana ili kuepusha migongano ya maslahi.

Alisisitiza, “Hunyanganywi mali yako wala kumkabidhi mwanao kwa kificho. Unatamka wazi, hoteli hii mali yangu, daladala 10 za Dar es Salaam kwenda Gongo la Mboto ni zangu.” Kwa mujibu wa Kikwete, sheria ya kuzuia wanasiasa hao kufanya biashara, itaepusha manung’uniko ambayo yamekuwa yakitolewa huku yakiwahusisha viongozi na shughuli mbalimbali.

“Manung’uniko ya watu tunayasikia (vinginevyo tunaishi dunia ya mbali) wanavyotuhusisha sisi na shughuli hii na shughuli ile. Ndiyo maana nimesema jambo hili tukae tulitafakari vizuri,” alisisitiza. Alisema Ibara ya 110 ya CCM inasisitiza suala la maadili na hivyo, mwaka huu, uwe wa kusimamia kikamilifu maadili ya viongozi wa chama na serikali.

Kuhusu uhusiano mbaya kati ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Kikwete alisema chanzo cha tatizo siyo chama chake kwa kuwa chenyewe kinaongoza nchi na hakina maslahi katika kugombana. Alisema CCM ina maslahi katika kupatana na ndiyo maana ilikuwa ya kwanza kupendekeza mazungumzo ya mwafaka kwa dhamira ya kubadilisha uhusiano huo wa kihasama ili uwe katika misingi ya kidemokrasia.

Katika kuelezea kukerwa kwake na siasa za chuki kugeuzwa mazoea, Rais Kikwete alisema baada ya mazungumzo yanayoendelea ambayo yako mbioni kukamilika, inabidi liwe fundisho ili hali hiyo isijirudie. Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa CCM amepiga marufuku wagombea katika chaguzi ndani ya chama hicho, kukusanya wajumbe kwa lengo la kuzungumza nao kabla ya uchaguzi kwa lengo la kuwashawishi wawapigie kura.

Alikuwa akizungumzia uchaguzi ngazi ya Jumuiya, unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. “Safari hii marufuku kumuita mjumbe yeyote. Na tutakuwa makini..mliozoea hayo muache, atakayeitisha huo mkutano uongozi hautaki,” alisema Kikwete.

Katika sherehe hizo, Kikwete alitaja majukumu saba ya msingi yatakayotekelezwa na chama chake mwaka huu kuwa ni pamoja na kutekeleza Ilani, kuimarisha uhusiano na vyama vingine vya siasa, maadalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kushiriki katika uboreshaji wa Daftari la Wapigakura, Kuendelea kusimamia maadili ya viongozi na uongozi, Uchaguzi wa jumuiya, na Kutekeleza mradi wa kuimarisha Chama.
 
Geee! Tumechoka na kauli zako zisizo na vitendo kila kukicha! Vunja baraza lako la mawaziri na mafisadi wote na waroho wa kujilimbikizia utajiri kupitia nyadhifa zao uwatose! Na wewe mwenyewe kama siyo safi ni bora ujitose tu! :(

“Hunyanganywi mali yako wala kumkabidhi mwanao kwa kificho. Unatamka wazi, hoteli hii mali yangu, daladala 10 za Dar es Salaam kwenda Gongo la Mboto ni zangu.” Kwa mujibu wa Kikwete, sheria ya kuzuia wanasiasa hao kufanya biashara, itaepusha manung’uniko ambayo yamekuwa yakitolewa huku yakiwahusisha viongozi na shughuli mbalimbali.

“Manung’uniko ya watu tunayasikia (vinginevyo tunaishi dunia ya mbali) wanavyotuhusisha sisi na shughuli hii na shughuli ile. Ndiyo maana nimesema jambo hili tukae tulitafakari vizuri,” alisisitiza. Alisema Ibara ya 110 ya CCM inasisitiza suala la maadili na hivyo, mwaka huu, uwe wa kusimamia kikamilifu maadili ya viongozi wa chama na serikali.


Wandugu hapa ndipo usanii ulipolalia hayo maadili ya viongozi naona kutakuwa hakuna chochote cha maana, bali ni kuendelea kuwalinda mafisadi.
 
It appears the message has been delivered loud and clear wanaJF na wahanga mbalimbali. Tusubiri kuona huo uadilifu.

BUT - nijuavyo ni kwamba hata sasa upo utaratibu (au ni sheria?)inayomtaka kiongozi kuorodhesha mali alizo nazo. Mara ya mwisho jambo hili lilipoandikwa magazetini, baadhi ya viongozi walikuwa wamesita kufanya hivyo, na hakuna lolote lililotendeka kuwawajibisha. Anzia hapo kwa kutekeleza utaratibu huo vizuri bila ya kusubiri hayo mengine yatakayochukua muda kuyatayarisha kabla ya kuyatekeleza.
 
Rais Jakaya Kikwete, amesema imani ya wananchi kwa viongozi inaanza kupungua kutokana na ukosefu wa uadilifu na uaminifu, hali ambayo inahitaji kushughulikiwa haraka kabla hali haijawa mbaya.[/QUOTE]

tueleze kipimo chako cha hali mbaya.

"Manung'uniko ya watu tunayasikia (vinginevyo tunaishi dunia ya mbali) wanavyotuhusisha sisi na shughuli hii na shughuli ile. Ndiyo maana nimesema jambo hili tukae tulitafakari vizuri,"

You are a joker....tukae tulitafakari..how long?

Mr JK unatoa hotuba nyingi na promise nyingi lakini no action yoyote...i wish 2010 iwe kesho
 
Ninachoona hapa kila mtu anafanya jitihada kujiwekea nafasi ya kupendwa zaidi na kujisafisha kwa migongo ya wengine,all in all ninakubaliana na Presidaa ktk jambo hili, ukimsikiliza anonyesha kukerwa na hali hii na kwakweli ni haki yake kuwa hivyo zaidi ya hapo kuna sura ingine hapa ,watu wanaanza kuona kuwa ni dhambi kiongozi kuwa tajiri hata kama hiyo hela kaipata kwa uhalali!

Yuko one step forward ktk jambo hili ingawaje itachukua muda kwa sisi kumuelewa.

Mheshimiwa kaza buti yako sfari ni ndefu na ngumu mno.
 
JF tumepiga kelele kwa miaka miwili sasa about JK cabinet, however tulionekana kama haters wa maendeleo. We point fingure about what need to be fixed, but JK acts like is def. Now he tries to play like he is outsider. Just give us the brake, its your mess you better clean it.
 
Je, alimtuma PM kuongea na mawaziri? Nchimbi anafanya kampeni kwamba Msabaha anataka kuondoka na PM, tusikubali yeye ndiye aliyefanya makosa!!!!!
 
Je, alimtuma PM kuongea na mawaziri? Nchimbi anafanya kampeni kwamba Msabaha anataka kuondoka na PM, tusikubali yeye ndiye aliyefanya makosa!!!!!

Kwi kwi kwi!!! kwahiyo wanataka kumtosa Msabaha sio? Nimesikia kuna maandamano mengine kesho huko Dodoma ya kumpongeza JK kuwa rais wa AU. Mwaka huu ni maandamano na safari, mambo ya uzalishaji na maendeleo yakae pembeni. Baadaye watatuambia uchumi umekua, labda kama uchumi huo wanaulisha GM food.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom