Viongozi wapya wa TUCTA sijui bado wako kwenye "honeymoon"!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,853
Viongozi wapya wa Shirikisho la Wafanyakazi Nchini(TUCTA),tangu wamechaguliwa na kutoa ahadi za kutatua matatizo ya wafanyakazi, wamepote jumla na wala hawasikiki kama wapo.

Binafsi nabaki najiuliza hivi hawa jamaa bado wanakabidhiana ofisi au hawa jamaa wapya bado wako kwenye honeymoon baada ya kushinda uchaguzi?

Matatizo ya wafanyakazi nani ayasemee kama sio nyinyi?

Watumiaji wa JamiiForums ndio wa kupaza sauti kwa kila kitu kinachoendelea hapa nchini?

Taasisi nyingi mbona hivi sasa ni kama vile zime-paralyse?

Kama hamna ujasiri madaraka mnayataka ya nini?

Ni wakati wa watu kwenda kuchunga ng'ombe na kuwaachia ofisi wenye uthubutu na ujasiri.
 
Bado wanatathmini akili za wanachama wao.Wakishazielewa kwa undani watatoa msimamo wao.
 
Back
Top Bottom