Kumekuwa na msuguano mkali sana kati serikali iliyopo madarakani na Vyama vya Upinzani. Vyama vya Upinzani vimekuwa vikilalamika kuwa vimehujumiwa sana hasa kwenye chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024. Kutokana na upande wa serikali kutotaka kukaa pamoja na Vyama vya Upinzani na kuzimaliza tofauti zao, baadhi ya vyama hivyo vya Upinzani vimeanzisha vuguvugu la kulazimisha mabadiliko. Pamoja na hayo, serikali bado haijaona umuhimu wa kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao.
OMBI LANGU KWENU viongozi wa Dini ni kwamba, ebu fanyeni utaratibu. Waiteni viongozi wa serikali kwa upande mmoja na upande mwingine viongozi wa vyama vya Upinzani. Ninyi mkiwa kama wapatanishi wakuu, toeni nafasi kwa kila upande kueleza dukuduku zake zote kisha jipeni muda ili kuchambua kwa kina maelezo ya kila upande, na mwishowe toeni majibu bila kupendelea upande wowote na yasimamieni makubaliano ya hizo pande mbili.
Nafikiri kwa kufanya hivyo mtakuwa mmetimiza wajibu wenu vizuri sana na Mungu atawabariki.
Ifahamike kuwa, tukiacha hizi pande kutunishiana misuli bila kusuluhisha, ipo siku hakutakuwa tena na fursa hiyo ya kuzikutanisha pande hizo kwa sababu maji yatakuwa yameshamwagika tayari.
Nawasilisha.