Viongozi wa yanga na Hersi wanavyoishi maisha ya maigizo yanga

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
Viongozi Yanga na Engineer Hersi wamefeli ahadi zao za kuipa ubingwa yanga...lakini GSM haijafeli kwa ahadi zake za kuipatia pesa Yanga...nianze kwa kusema Yanga ni timu iliyo na nguvu kubwa ya mashabiki hapa nchi hivyo basi kila anaeingia yanga hubadili mtazamo wake na kuingia na tamaa ya maslahi binafsi..kwanini nimesema Engineer kafeli.

Hersi ndio mtu pekee ambaye GSM imemuamini na kumpa majukumu ya kusimamia klabu kimaono na mafanikio..GSM pamoj na wadhamini wengine wa yanga wameweka pesa kwa ajili ya timu huku macho yao yakielekezwa kwa Hersi kwakuwa wao hutaka matokeo chanya.

Katika kufanya hivyo hersi alisimama na timu kwa msimu wa 19/20 kwa nia ya kujenga timu ambayo wachezaji wake walikuwa sio na hadhi yakuchezea yanga mfano yikpe na wenzake hivyo basi mashabiki wa yanga waliamini timu kuwa ifikapo 20/21 timu itabadilika matokeo yake timu ilisajili wachezaji zaidi ya 14 baada ya usajili engineer akatoa ahadi kuwa yanga ikishindwa kuchukua ubingwa aulizwe yeye bila kusahau alisajili wachezaji wenye level ya kawaida sana ambao sio wa kuipa ubingwa timu bali ni wakuleta ushindani wa ligi tu.

Nirudi kwa viongozi wamekuwa hawana msimamo wa kiutendaji inafikia wakati majukumu yote ya klabu bila hersi kutoa go ahead hakuna anaeweza kuamua na kumbuka sakata la simon alipewa kesi na shutuma nyingi ila alivyokuja kusafishwa nashangaa hakupewa nafasi yake ya kaimu katibu mkuu wakati aliyekuwa kwenye hiyo nafasi aliwekwa kwa muda kama ilivyo simon hapo kuba shida..

mithali kashinda kesi alitakiwa kupewa majukumu yake yote hili tuliangalie kwakina nani kabeba interest hiyo..timu inapofanya vizuri watu hupeleka sifa kwa engineer lakini timu ikikosea tu engineer hujivua na lawama hupelekwa kwa msolla ambaye kutokana na njaa zake amewezwa kutulizwa na nguvu ya pesa.

Uongozi na hersi umegawa timu ya yanga waliangalie kuna wachezaji wanapendwa na hersi na kuna wachezaji wanapendwa na uongozi wa klabu ila kama kweli wana nia yakuvukisha yanga kuchukua ubingwa basi wanatakiwa kukaa pembeni ili watu wenye weledi wa kuongoza klabu waweze kusimamia kwani ukiangalia sisi watanzania tunapenda sana umbea hivyo wrngi macho yao yapo kwenye social media na viongozi wengi ikiwemo hersi wameshanunua waandishi nia na madhumuni ni kumtaja kwa mazuri tu yakija mabaya wana kimbizia kwa msola ila kuna klabu gani wasemaji wawili hili nalo tatizo linatakiwa kuangalia hawa wasemaji wawili ukifatilia hawatoweza kukaa zizi moja kwasababu ni kazi ya mtu mmoja ila kwa kuwa watu wanajengea bomoa klabu hawawezi kuliona..

Hersi kauli yako mwenyewe unaipinga katika vyombo vya habari kusema yanga tunaifananisha mafanikio na simba unasahau ahadi zako ulizoahidi maana yake uliwaaminisha mashabiki timu inaweza leo unakuj unatoka katika media nakusema kuwa tusilinganishwe na simba kimafanikio usipreach politics kwenye mpira Yanga umeikuta na hii tanga utaiacha hata kwa viongozi wengi kwasababu nyie ndio mnamfanya GSM aonekane kafeli kwa uzembe wa asilimia kumi na kutaka madaraka zaidi.

Avic town imegeuzwa maskani kwa viongozi daily kushinda wakiangalia mazoezi thats very wrong na ndio mana baadhi ya wachezaji hawaheshimu viongozi kwa kuwa mnashinda nao tuliangalie kwa kina hili vile vile unataka kutuaminisha kuwa usajili unafanya kwa mapendekezo ya namna gani je ni chini ya kamati ya usajili!?

GSM angalieni kuhusu Hersi na watu aliowaweka mkipeleka auditing mtawachukulia sheria ila kama GSM wanataka kufika mbali na Yanga wampangie majukumu mengine Hersi kisha waangalie namna watakavyopata mtu sahihi anaeendana nao katika biashara hii ya kusimamia Yanga so far Yanga itachukua Azam Cup ila sio kigezo cha kufanya timu ionekane imefanya vizuri hizo ni juhudi za mashabiki nje ya uwanja.

Tunawapenda GSM naomba mlichukulie hatua kabla brand yenu haijavunjiwa heshima...GSM nikubwa kuzi mtu..mkisikiliza interview ya hersi EFM utagundua muda wake wa kuwavukisha mnapotaka umefikia tamati.

ifike wakati tutambue kuwa Yanga ni kubwa na pia tutambue kuwa usimamizi mbovu..GSM msikate tamaa ya kuwekeza ndani ya Yanga bali mjue pia anaewafelisha ni mtu wenu tu...Tunaomba GSM kabla ya kusajili mpewe finanvial report zote za msimu huu matumizi na usimamizi wa klabu vile vile muone je mtaivukisha yanga sisi kama mashabiki tumechoka kuahidiwa kila msimu.

Tunawapenda GSM.
Hakuna mtu mkubwa kuzidi GSM na YANGA
wako
HRN
 
Hao GSM hawawezi kuipa Yanga kile Mo anachofanya Simba, wachezaji wanaowaleta Yanga wengi ni wa bei chee wengine wanatolewa kwa mikopo kwenye timu zao.

Kuendelea kuwaamini GSM watawapa mafanikio Yanga ni kujidanganya, hao GSM waombe Mungu Manji aje kuwasaidia labda ndio mtasogea mbele kidogo, lakini wenyewe hawawezi ni story tu, hawawezi kulipa aina ya mishahara MO anayolipa wachezaji wa Simba SC.
 
Hao GSM hawawezi kuipa Yanga kile Mo anachoganya Simba, wachezaji wanaowaleta Yanga wengi ni wa bei chee wengine wanatolewa kwa mikopo kwenye timu zao, kuendelea kuwaamini GSM watawapa mafanikio Yanga ni kujidanganya, hao GSM waombe Mungu Manji aje kuwasaidia labda ndio mtasogea mbele kidogo, lakini wenyewe hawawezi ni story tu.
Sasa mpaka umtaje Moo
 
Nini maoni yako kuhusu kugomea mechi dhidi ya simba ile tar 8 na yanga kuendelea kukakataa kuingiza timu tar 3
 
Je'Hersi ni mtu wa mpira na ana uzowefu wa ligi ya Bongo mpaka apewe majukumu makubwa kwenye club kubwa kama Yanga?
Kwenye kinyang'anyiro cha kusaka ubingwa wa vpl kwenye hizi timu mbili kubwa Simba na Yanga huwezi kumtanguliza Hersi akachuwane na mtu kama Hans pop,Magoli n.k,hasa ukizingatia mpira wa bongo figisu za nje ya uwanja ni pana sana kuliko ndani ya pitch.
 
Hao GSM hawawezi kuipa Yanga kile Mo anachofanya Simba, wachezaji wanaowaleta Yanga wengi ni wa bei chee wengine wanatolewa kwa mikopo kwenye timu zao.

Kuendelea kuwaamini GSM watawapa mafanikio Yanga ni kujidanganya, hao GSM waombe Mungu Manji aje kuwasaidia labda ndio mtasogea mbele kidogo, lakini wenyewe hawawezi ni story tu, hawawezi kulipa aina ya mishahara MO anayolipa wachezaji wa Simba SC.
Kwani mchezaji kucheza kwa mkopo ni tatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom