Viongozi wa upinzani wajiuzulu Uingereza

Viongozi wa upinzani wajiuzulu Uingereza

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,548
Kiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza Ed Miliband amewaambia wanaharakati wa chama hicho kwamba anajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho kufuatia matokeo duni ya uchaguzi mkuu.

Miliband ambaye amempongeza Waziri mkuu David Cameron kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili amesema kuwa anachukua jukumu la kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo. Chama cha leba kilishindwa vibaya katika uchaguzi huo. Katika hotuba aliyotoa mjini London,Miliband alisema kuwa ni wakati mtu mwengine anafaa kuchukua uongozi wa chama hicho huku akithibitisha kuwa naibu kiongozi wa chama hicho Harriet Harman atashikilia uongozi kwa mda.


Bwana Miliband alipongezwa na wafanyikazi wengine alipowasili katika makao makuu ya chama cha leba katikati mwa London

Wakati huohuo Nick Clegg amejiuzulu kama kiongozi wa chama cha Liberal Democrat kufuatia matokeo yalioonyesha kuwa chama cha Conservative kinaelekea kushinda uchaguzi huo (Kimeshashinda tayari)


Chanzo: BBC Swahili

Nionavyo:
Huu ni wakati wa kujifunza kutoka kwa wenzetu...ukishindwa unaachia wengine na si kung'ang'ania kuongoza na kugombea nafasi uliyoshindwa tena na tena.
 
Habari ndio hiyo..

Mkuu ningependa kuona vyama vyetu vinapractice demokrasia kama wafanyavyo wenzetu....hapa kwetu utaambiwa hawa waliopo ndio wanaimarisha chama...kwa hiyo waendelee tu kuongoza.
 
viongozi wenyewe wakina MREMA!! Juzi amesikia fununu za kutaka kufukuzwa, heee akawa time wote c wanachama tena!! kwani afrika siasa tumeifanya kama njia ya kuendesha maisha yetu, ni vigumu kufanya hayo mambo, hadi mwisho wa dunia, kwa afrika itakuwa ngumu,
 
Ajiuzuru tu. Kaka yake alikuwa na akili kuliko yeye wakamtoa. David angeongoza vizuri Labour
 
viongozi wenyewe wakina MREMA!! Juzi amesikia fununu za kutaka kufukuzwa, heee akawa time wote c wanachama tena!! kwani afrika siasa tumeifanya kama njia ya kuendesha maisha yetu, ni vigumu kufanya hayo mambo, hadi mwisho wa dunia, kwa afrika itakuwa ngumu,

Mkuu mbona umekata tamaa kabisa....kizazi cha .com kinaweza badili hali ya mambo
 
Umemsahau Nigel wa UKIP nae kaachia ngazi

Wotee mkuu.....na hii ndio demokrasia ya wazi kabisa...ukishindwa unakaa pemben...wengine wanaendeleza....nyumbani hapa majanga
 
Wotee mkuu.....na hii ndio demokrasia ya wazi kabisa...ukishindwa unakaa pemben...wengine wanaendeleza....nyumbani hapa majanga

Nyumbani hamna mshiko ndio maana mi sio mshabiki wa vyama ila UK ni conservative
 
Nyumbani hamna mshiko ndio maana mi sio mshabiki wa vyama ila UK ni conservative

Opinion poll safari hii imeenda halijojo....matokeo ya safari hayakutegemewa kabisa kama conservative wangekamata majority in parliament
 
Opinion poll safari hii imeenda halijojo....matokeo ya safari hayakutegemewa kabisa kama conservative wangekamata majority in parliament

Kwa kweli ni pigo kwa vyama pinzani, hawakutegemea.
Mpaka kujiuzulu imewauma sana, hata George gallaway kajiuzulu pia, jamaa nilikuwa namkubali sana
 
Kwa kweli ni pigo kwa vyama pinzani, hawakutegemea.
Mpaka kujiuzulu imewauma sana, hata George gallaway kajiuzulu pia, jamaa nilikuwa namkubali sana

Ila kule Uskochi SNP wamefanya kufuru
 
Back
Top Bottom