Habarini za jion wanajukwaa...!
Naombeni viongozi wa UKAWA taifa pamoja na wale wa Kanda kulitatua hali ya sintofahamu kwa watu wa jimbo la Mtama.
Kwa kifupi ni aliyekuwa mgombea wa Ccm kabla ya Kura za maoni ndg Selemani Methew Luwongo baada kukosa Kura za maoni kupitia Ccm hatimaye alitangaza kuwa atahamia Act-Wazalendo siku ya trh 10/08/2015 lakin jambo la kushangaza alikuja Mtama trh 11/08/2015 na kutangaza kuwa maamuzi ya Kuhamia Act-Wazalendo atayafanya trh 14/08/2015 baada majina kutoka ya wagombea Ubunge kupitia CCM.
Trh 15/08/2015 aliamua Kuhamia CHADEMA na kuikacha Act-Wazalendo Hilo halikuwa tu jambo la kushangaza lakini pia liliwashtua baadhi ya wafuasi wake.
Baada ya Kuhamia CHADEMA huyu jamaa anamlazimisha mgombea Ubunge kupitia CUF ndg Mchinjita amuachie nafasi huku akisema kuwa katumwa na mamlaka ya juu, jamaa alipoona ndg Mchinjita anaweka ngumu akaanza kueneza Habari za uongo kwa wanamtama kuwa Mchinjita ni kambi ya Membe na kusema kuwaambia wanamtama kuwa trh 16/08/2015 angekuja ndg Godbless Lema na Freddy Lowassa kuzungumza na Mchinjita ili ikiwezekana Mchinjita apewe pesa aache jimbo. Huu ni uzushi na uongo aliousema ndg Selemani Methew Luwongo kwa wananchi wa Mtama.
Kilichonisukuma kuandika haya ni kitendo alichokifanya ndg Selemani Methew Luwongo leo trh 18/08/2015 kuamua kuja kufanya mkutano wa hadhara na kutangaza kuwa anachukua fomu ya Ubunge na jumapili anaanza kampeni pia mwenyekiti wa wilaya ndg Chikawe kutangaza hadharani kuwa kusini hapa jimbo la Mtama hakuna Ukawa hivyo kumuambia ndg Selemani Methew Luwongo achukue fomu.
Wanaukawa tunaenda wapi huku mbona tumeshamla ng'ombe mzima bado mkia tu...? Ndg Maalim Seif nasikia leo ulikuwa Mchinga nakuomba ututembelee Mtama uje utoe ufafanuzi na kama hapa mtama hakuna Ukawa naomba utuambie.