Viongozi wa TUCTA nitawashangaa mkimualika "Mkulu" kwenye sherehe za Mei Mosi mwaka huu wa 2017

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,917
Ameonyesha kutojali kundi hili kwa kiasi kikubwa sana na mbaya zaidi siku hizi hata haongelei kabisa maslahi yao.Yaani ni kama vile hawamuhusu.

Kundi hili limebaki kama yatima. Hawajui ni lini watapandishwa madaraja,hawaelewi ni lini watalipwa malimbikizo yao ya mishahara,nk.Ni huruma tupu kwa hawa wenzetu.

Kama Mkulu ataendelea na msimamo wake huu mpaka mwezi Mei na nyinyi viongozi wa TUCTA mkampa mwaliko kuwa mgeni rasimi kwenye sherehe za Mei Mosi, basi mtakuwa ni watu wa ajabu sana.

Kama mbwai na iwe mbwai tukutane 2020.
 
Taifa hili halina chama cha wafanyakazi kuna waoga na wachumia tumbo tu waliojivika cheo cha TUCTA hawa wanajali maslahi yao na familia yao,hata hivyo ni Taifa hili pekee mambo yanamna hii yanatokea
Hasa CWT ndio Waoga wakutupwa, halafu hawajitambui
 
usipomualika rais utamualika nana? Ni nani unadhani takuwa na majibu ya maswali ya wafanyakazi!! Rais ni mtu sahihi,,sema kutomualika rais ni ishara kuwa amkubaliani na namna anatatua changamoto zenu!!!
 
Sioni hata faida ya hii kitu inaitwa TUCTA, haina faida yoyote kwa mfanyakazi, zaidi viongozi wake kushibisha matumbo yao hadi kusahau wajibu wao. Kila kukicha wafanyakazi wanalia kwa uonevu/ukandamizaji/unyonyaji unaofanywa na serikali hii lakini sisikii TUCTA wakisema chochote, kana kwamba hawapo. Kwa ujumla sioni umuhimu wa hili shirikisho, mimi naona lingefutwa tu.
 
TUCTA hamna kitu kabisa wameshindwa hata kuwatetea wafanyakazi kuhusu kutoka 8% hadi 15,upandaji wa madaraja,uhaba wa watumishi
 
Sasa wasipomualika tutapata wapi pa kusemea!!? Au unataka nalo hilo liwe sababu ya kutopandishwa mishahara?? Lazima aalikwe hakuna namna
 
usipomualika rais utamualika nana? Ni nani unadhani takuwa na majibu ya maswali ya wafanyakazi!! Rais ni mtu sahihi,,sema kutomualika rais ni ishara kuwa amkubaliani na namna anatatua changamoto zenu!!!
Wamualike hata mzee Mwinyi Ali Hassan
 
Mzee wa vinyongo na visasi asipoalikwa lazima alipize!!

Hivi hii nchi vyama vya wafanyakazi vipo kweli!!! Na vinafanya nini haswa? Upuuzi tu.
 
Sioni hata faida ya hii kitu inaitwa TUCTA, haina faida yoyote kwa mfanyakazi, zaidi viongozi wake kushibisha matumbo yao hadi kusahau wajibu wao. Kila kukicha wafanyakazi wanalia kwa uonevu/ukandamizaji/unyonyaji unaofanywa na serikali hii lakini sisikii TUCTA wakisema chochote, kana kwamba hawapo. Kwa ujumla sioni umuhimu wa hili shirikisho, mimi naona lingefutwa tu.
Wanazidi kutunyonya kwa kukata pesa yetu halafu hawafanyi lolote mishahara haipandi watu hawapandishwi madaraja wao wapo busy kukata pesa yetu wezi wakubwa hawa bora wasiwepo
 
Salary Slip pole sana mkuu, sijui Lowasa alikuaidi cheo gani..... Inaonekana ushindi wa Magufuli umekuharibia sana malengo yako kisiasa.
 
Back
Top Bottom