Viongozi wa Tanzania are you serious????

kkiwango

Senior Member
Aug 27, 2007
173
14
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kuwa vijana hawafanyi kazi, saa nne asubuhi wapo wanacheza pool. maswali yangu kwa viongozi wa nchi hii ni....

1. Je mmetenegeza nafasi au kuhakikisha nafasi za hao vijana kufanya kazi zinapatikana? nitatoa mfano wa jinsi Uhamiaji na wizara ya kazi mnavyorudisha nyuma ndoto ya kusaidia vijana kupata kazi, idara hizi mbili licha ya maagizo na mabadiliko kadhaa ya uongozi katika utendaji sijaona mabadiliko, wageni wasio na sifa wanapata vibali vya kufanya kazi mpaka za administration kwenye mashirika binafsi ili hali kuna vijana wengi wa kitanzania wenye kuweza kufanya kazi hizo na zaidi.

Shirika dogo la waajiriwa 9, wageni ni watano (5) kweli vijana wasicheze pool kwanini? au ndio tunataka wakatukabe huko mitaani? Hebu kuweni serious nyie mliopewa dhamana ya kuongoza wananchi acheni bla bla fanyeni kazi zenu. Kwanini msijifunze kwa nchi kama Ethiopia? hawakubali ujinga wa namna hii.......afu wakati huo huo mnataka kurudishiwa pesa za mkopo wa elimu.....are u serious??????? vijana watoe wapi hizo pesa wakati mnawabana wasipipate kazi za kuajiriwa?.

2. Vijana wajiendeleze na kuwa wajasiliamali......very good idea, lkn je elimu mliyowapa inawasaidia wao kujiajiri? au walipewa elimu ya kuja kuajiriwa? vijana hao hao wakijitahidi kubuni miradi yao, mabank hayawapi pesa eti hawaaminiki au hawana dhamana (mfano mali isiyohamishika) sasa tunataka vijana wafanye nini jamani........ wajifungie ndani wawe mazezeta? wakilima hakuna masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo (ni mpaka uwe na mtaji mkubwa ulime kisasa uje kuuza nje ya nchi)

Viongozi kuweni serious muangalie hili suala la vijana kwa nyuzi 360.....
 
Back
Top Bottom