Viongozi wa Simba hamna cha kujitetea mmevurunda toka usajili

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Hakika Viongozi wa Mabingwa wa Soka Simba mmetuudhi sana wanachama ,wapenzi na mashabiki wenu kwa matokeo ya juzi.

Usajili mmefanya kinyume na matakwa ya kocha mkuu,Wachezaji muhimu kama Emmanuel Okwi,Haruna Niyonzima na Kotei mnawaacha mnaenda kutuletea watalii toka Brazil Aibu kubwa matokeo ni timu kushindwa kufuzu.

Kama klabu zetu zinalalamika ubovu wa viwanja hao Wabrazil watacheza kweli?Tanzania haijafikia hatua ya kusajili nje ya Afrika,Yanga ilileta wabrazil je walifanya nini cha ajabu.

Ukweli Viongozi wa Simba maswala ya Wachezaji mwachieni Kocha ,sidhani kama kocha hakuwahitaji kina Okwi,Kotei na Niyonzima,au kama kocha aliagiza hao Wabrazil.

Kama kweli Simba inataka kutetea Ubingwa wake basi iangalie upya Usajili wake vinginevyo Ubingwa utavuliwa mapema.
 
Umeongea ukweli kabisa.
 
Mwakani tukienda na wachezaji hawa kwa kufanya marekebisho kwa kusajiri ma strikers wawili wa maana tutafika mbali.

Ombi langu si kila msimu unabadilisha kikosi yaani wachezaji wanakaa muda mfupi kuendea mashindano makubwa wanashindwa kuzoeana kwa wakati kama tulivyofanya msimu huu viongozi acheni kabisa kusajiri timu upya kwa pressure za mashabiki
 
Simba timu nzuri wanayo, waliwadharau UD Songo kipindi cha kwanza ikawaletea ugumu. Hata goli la UD Songo ni makosa ya Kagere kutoka na kuacha mwanya wa goli. Vinginevyo Simba ndio iliyocheza na kutawala mchezo. Kazi nzuri iliyofanywa na mabeki wa UD Songo ndio iliwanyima ushindi Simba.
 
Haya Ni Matokeo Ya Kusajili Majina Badala Ya Watu Wa Kazi,
Huwezi Acha Wachezaji Kama, James Kotei Kiungo Mkabaji Ukabaki Na Wachezaji Aina Moja Ktk Safu Ya Viungo.

Huwez Muacha Mtu Kama Emmanuely Okwi, Mchezaji Anaeweza Kukupa Matokeoa Muda Wowote Kwa Uwezo Wake Binafsi, Alafu Ukaenda Kusajili Watu Wanakuja Kukaa Benchi, Hizo Hela Ulizotumia Kwa Uliowasjili C Bora Ungefanya Kuwanakiza Ulokuwa Nao, Waliokupa Kitu Msimu Uliopita, Angalia Sasa Aibu Iliyowakuta, Imewaumbua.

Simba Ile Ya Msimu Uliopita Iliyofika Robo Fainal , Ingebaki Na Wakongezwa Watu Wachache Tu Kuziba Mapungufu Yaliyokuwepo.
 
hivyo visingizio huwa vipo tu team ikifungwa
in short mbumbumbu mlizidiwa tu uwezo na Ud songo
 
Simba wanatakiwa wawe na scout professional kabisa wanao ujua mpira wa Africa na ligi zake na si kuwaachia hawa wasaka tonge akina hans pope,hawajui lolote kuhusu mpira wapo pale kupiga hela za MO.Kama wale wa Brazil ni mzigo tu kwa Club.
Alafu si kila mwaka unatakiwa ufanye usajili,misimu mingine kama mna kikosi kizuri mnaongeza mmoja au wawili basi.
 
Back
Top Bottom