PreGE2025 Viongozi wa NCCR Mageuzi wilaya ya Magu wakibwaga chama na kuhamia ADC

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Katibu wa NCCR Mageuzi Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Robert Busumabu na mwenzake Mwenyekiti wa Vijana wilaya hiyo, Mathayo Ndalahwa wamehamia chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) huku wakieleza sababu za wao kuhama.

Mara baada ya kupokelewa na Kamishna wa ADC Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Mrisho viongozi hao wamesema kuwepo kwa ahadi nyingi zisizotekelezeka, viongozi na wanachama kufukuzwa au kusimamishwa kiholela na kutokuridhishwa na sera za chama hicho zimewafanya kuachana nacho.

"Nimekuwa katibu wa NCCR Mageuzi jimbo la Magu kwa muda wa miaka miwili, nimekaa kwenye chama hicho lakini baadhi ya mambo mengi yalikuwa hayanifurahishi hususani kuahidiwa ahadi zinakuwa hazitekelezeki pili wanachama au viongozi kufukuzwa au kusimamishwa pasipo sababu za msingi lakini pia Sera zake sio ndio maana nimeamua kutoka na kuhamia ADC," amesema Busumabu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akiunga mkono hoja hizo Mwenyekiti wa Vijana NCCR Mageuzi wilaya hiyo, Mathayo Ndalahwa amesema mbali na sababu hizo lakini pia amevutiwa na sera za chama cha ADC hali iliyompelekea kuhama.

"Nimeamua kujiunga na chama hiki kwa sababu ya ahadi za chama nilichokuwa kuwa zinatolewa lakini hazitimii lakini pia sera za ADC zimenivutia ndio maana nimeamua kujiunga na chama hiki sijashawishiwa na mtu wala kulazimishwa na mtu ni moyo wangu umeamua kwa mapenzi ya dhati," amesema Ndalahwa

ni muhimu sana wanainchi kutumia vyema uhuru na haki zao za kikatiba bila woga 🐒
 
Kichekesho, wanazunguka mulemule ndani, ingependeza sana wangeenda hata ACT kama si ccm kama ilivyozoeleka. ADC ni chama kidogo sana hakina mvumo
 
Back
Top Bottom