Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Viongozi wa jamii ya kimasai nchini (Malaigwanani) wametoa msimamo wao wa kumchagua tena rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendelea kuongoza nchi kwa miaka mitano ijayo kutokana na utendaji kazi wake.
Akizungumza baada ya kikao kilichowakutanisha viongozi hao kutoka Siha na Longido, mwenyekiti wa Malaigwanan Tanzania, Joseph Ole Paserian amesema jamii hiyo imeridhishwa na kazi zilizofanywa na Rais Samia na hivyo watahakikisha wanahamasishana ili wanajamii wa kimasai wajitokeze kupiga kura kumchagua Rais Samia.
Aidha katika kikao hicho pia wameiomba serikali kupitia Kampuni ya ranchi za taifa (NARCO) kurudisha kwa jamii hiyo eneo ambalo walikua wakitumia kwa malisho kabla ya kupewa mwekezaji jambo ambalo linawaweka katika hatari ya kukosa malisho ya mifugo.