Viongozi wa JK walisoma history?

Viongozi wa JK walisoma history?

Joined
Apr 3, 2012
Posts
28
Reaction score
7
Ndg wana jamvi kwanza nianze kwa kuwatakia ndugu zangu wote walio kwenye mfungo ramadhani njema,sisi sote ni ndugu na kwa wale ambao hamjafunga muonyeshe ushirikiano kwa wenzenu ili tudumishe amani na mshikamano.

Nirudi kwenye mada, kwanza kwa wale wanafunzi wa form one ukimuuliza what is history atakwambia Is the study of the past,prent and future event, lakini ukiendelea mbele zaidi uapata maana ya History ni somo la makosa ya mbele ili yasijirudie tena ktk kizazi hiki na kijacho.

Kwa Tanzania mfano kina chiefu Mangungo tunasoma history walisainishwa mikataba kwa kuambiwa andika 111 kuwa ndio saini kumbe ni mkataba wa miaka miamoja kumi na moja,hili lilifanyika kwasababu hawakujua kusoma na kuandika ndio maana waliingia mkenge huo kwa kuuza nchi miaka hiyo.

History sasa inarudi kwetu ili tusirudie makosa hayo ambayo waliyafanya wazee wetu,sasa iweje leo mawaziri wetu wanasaini mikataba ya miaka mia moja,ina maana history hawakusoma au wanakariri kama vijana wa form one?Inakuwaje wanaambiwa wasaini hapa 100 kama hawakwenda shule?

Naomba kuwasilisha hoja ili tuijadili tuone kama in tija kwa taifa
 
Walisoma ndio. Si unasikia wengine wanasema kuwa Tanzania ni muungano wa Tanganyika na visiwa vya Unguja na Zimbabwe.
 
Back
Top Bottom