GE2025 Viongozi wa Dini watakiwa kukemea rushwa uchaguzi mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Viongozi wa dini, wazee wa mila na asasi za kiraia wametakiwa kushirikiana kwa karibu katika kupambana na vitendo vya rushwa wakati huu taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu, ili kusaidia jamii kupata viongozi bora, waadilifu na wenye kuzingatia masuala ya haki, uongozi na maendeleo ya wananchi.

Wito huo umetolewa na Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi, Stewart Kiondo, alipokuwa akifungua semina ya mafunzo kwa wadau hao, iliyofanyika mkoani Katavi kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya nafasi yao katika mapambano dhidi ya rushwa kipindi cha uchaguzi.

Kiondo amesema kuwa Ibara ya 9(h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza mamlaka na taasisi zote kuhakikisha zinachukua hatua madhubuti za kutokomeza rushwa, jambo ambalo limepewa nguvu pia na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329, hasa kupitia Kifungu cha 7(b) na Kifungu cha 15, vinavyolitaka TAKUKURU kuhamasisha ushiriki wa wananchi na taasisi nyingine katika mapambano hayo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesisitiza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutumia busara na hekima kukemea vitendo vya wagombea wanaojipatia umaarufu kupitia ahadi za miundombinu au misaada ya kifedha, jambo ambalo ni mwanya wa rushwa ya uchaguzi.

Aidha, ameonya juu ya tabia ya baadhi ya wananchi kuwa na kauli kama “unatuachaje?” pindi wagombea wanapokuwa tayari wamepita au kuchaguliwa, akieleza kuwa hiyo ni sehemu ya kushabikia rushwa na kuharibu misingi ya uchaguzi huru na wa haki.

Kwa upande wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Nassoro Kakulukulu, akizungumza kwa niaba ya washiriki wa semina hiyo, amesema mafunzo hayo yametoa mwanga mpya kuhusu wajibu wa viongozi wa kijamii katika kulinda maadili ya uchaguzi.
 
Viongozi wa dini, wazee wa mila na asasi za kiraia wametakiwa kushirikiana kwa karibu katika kupambana na vitendo vya rushwa wakati huu taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu, ili kusaidia jamii kupata viongozi bora, waadilifu na wenye kuzingatia masuala ya haki, uongozi na maendeleo ya wananchi.

Wito huo umetolewa na Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi, Stewart Kiondo, alipokuwa akifungua semina ya mafunzo kwa wadau hao, iliyofanyika mkoani Katavi kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya nafasi yao katika mapambano dhidi ya rushwa kipindi cha uchaguzi.

Kiondo amesema kuwa Ibara ya 9(h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza mamlaka na taasisi zote kuhakikisha zinachukua hatua madhubuti za kutokomeza rushwa, jambo ambalo limepewa nguvu pia na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329, hasa kupitia Kifungu cha 7(b) na Kifungu cha 15, vinavyolitaka TAKUKURU kuhamasisha ushiriki wa wananchi na taasisi nyingine katika mapambano hayo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Rushwa anazotoa Samia The Killer mchana kweupe (hata kwa viongozi wa kidini) nani anazishughulikia?
 
Screenshot_20250721-124551.png
 
wakaongelee madhabahuni au wasiongelee madhabahuni? kama wakikemea rushwa madhabahuni hamuoni kama wanafanya siasa madhabahuni? kama jibu ni sio, kukemea rushwa kuna tofauti gani na kukemea utekaji na uuaji? oneni aibu, pale mlipokosea jisahihisheni, kirini kwamba mliteleza,muanze upya, pengine mtasamehewa.

watu walikemea maovu, mkawafungia makanisa, mkawapiga virungu,mkawatoa damu, na kuwazuia kuabudu hadi leo. na leo mnarudi tena kwa viongozi wa dini. kama ninyi peke yenu ndio mliamini mnaweza kukemea maovu, na mkaweza, kwanini mnawageukia wao tena? Mungu na awahukumu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom