Viongozi wa dini wameona, kweli serikali bado?

K M S

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
524
424
Leo tumekua ibadani kumwabudu Mungu mchungaji kalitangazia kanisa kua kulingana na hali halisi ya ukame mchana waleo kutakua na maombi viwanja vya furahisha hapa mwanza kwa makanisa yotekuombea mvua na kumsihi Mungu atuepushe na baa la njaa linaloelekea kuikumba nchi kwani kuna maeneo tayari mifugo inakufana watu hawana chakula nimeskia na Bakwata pia wametangaza swali langu kama viongozi wameanza kunusa hatari je serekali bado hai hisi chochote kweli ili itoe anhalau tamko tu hata lakujihadhari
 
Matamko yameshatolewa muda mrefu kuanzia ziara zote za Waziri Mkuu na Za Rais. Labda halikueleweka tu ila tayari muda mrefu. TMA ambayo ni taasisi ya Serikali ilishatoa utabiri tangu mwezi Oktoba 2016.
 
Matamko yameshatolewa muda mrefu kuanzia ziara zote za Waziri Mkuu na Za Rais. Labda halikueleweka tu ila tayari muda mrefu. TMA ambayo ni taasisi ya Serikali ilishatoa utabiri tangu mwezi Oktoba 2016.
Ila mkuu alisema nchi haina njaa na haina shamba la kulima kugawia watu chakula...baada ya kauli hiyo ya mkuu ndio na viongozi wa dini wanatoka live kutuambia waamini wao tumwombe mungu wetu na tusimtegemee mwanadamu mkulu aliyepewa dhamana.
 
Watu wakiendelea kuimba wimbo huo, kweli itatokea. Kuna njaa na kutakuwa na njaa!
 
Sitashangaa kusikia serikali imepiga marufuku madhehebu ya dini kufanya maombi ya kuomba mvua
 
Jamani ndio maana MTU akisema tumuombee tufanye hivyo inawezekana mwenzetu anamatatizo makubwa ingawa tunaona LA kawaida
 
Back
Top Bottom