Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,357
- 23,759
Ndugu zangu Watanzania,
Watu wanakwenda kwenye nyumba za ibada kusikiliza neno la Mungu na siyo kwenda kusikiliza hisia za mtu na mtizamo wake wa kisiasa au mapenzi yake kwa chama fulani cha siasa. Watu wanakwenda kupata chakula cha kiroho na siyo kwenda kusikiliza uwanaharakati na habari za harakati katika madhabahu.
Kuna baadhi ya viongozi wa Dini wamesahau kabisa wajibu wao wawapo katika madhabahu na nyumba za ibada . Badala yake yamejivika uanaharakati na kujibika kengele shingoni mwao pamoja na kuwa vipaza sauti vya wanaharakati walioishiwa hoja na kufirisika kifikra. Kuna baadhi ya viongozi wa Dini wanahuburi siasa na kuleta michanganyo mpaka mtu unajiuliza ikiwa upo ni kanisani ama upo kwenye vikao vya chama ama kwenye mikutano ya kampeni.
Wengine wanafikia kuanza hadi kutoa matamko ya kisiasa ama kukariri Makelele ya Viroja vya wanaharakati waliokosa muelekeo na kutaka kuishinikiza serikali ama kuleta upotoshaji kwa umma. Wengine wamekuwa wakibebeshwa ajenda na wanaharakati ili wakaziongelee kwenye nyumba zao za ibada.
Chakusikitisha zaidi ni pale unapoona mazungumzo yao yakikosa msingi wa hoja zao wala kueleweka wanataka nini na kipi hawatakaa zaidi ya kudakia tu vijimaneno vya wanaharakati na wale maadui zetu wenye lengo Baya na Taifa letu.
Wengine wamekuwa wakizungumza mambo yenye kuleta uchonganishi kwa wananchi dhidi ya serikali yao. Rai yangu ni kuwaomba viongozi wetu wote wa Dini kujikita katika kuhubiri neno la Mungu na siyo hisia zao binafsi. Vitabu vitakatifu ndio uwe muongozo wao na siyo mapenzi yao binafsi kwa vyama vya siasa. Waache mara moja kuleta uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini wao ili waichukie serikali yao.
Wazungumze kwa vifungu na kuvirejea kama vilivyoandikwa na siyo kudakia matukio. Kazi ya kiongozi wa Dini siyo kuanza kutafuta umaarufu mitandao aka kutaka sifa. Kazi ya kiongozi wa Dini ni kufundisha upendo ,amani ,umoja , mshikamano, kusameheana na unyenyekevu. Ni kazi ya kiongozi wa Dini kuipomya mioyo iliyojeruhiwa ,kuumizwa na kuifundisha namna ya kusamehe na kufungua ukurasa mpya.
Siyo vyema kiongozi wa Dini kuanza kupandikiza chuki ,uhasama ,vinyongo ,visasi,maripizi ,mivutano na migogoro ya aina yoyote ile katika mioyo ya waumini.
Lakini pia viongozi wa Dini wajue kuwa wao ni wanadamu na siyo watakatifu au Miungu. Wao pia wanakosea na hawajakamilika. Hivyo wasijihesabie haki na ukamilifu.wasijipe haki ya kukosoa pasipo kukosolewa. Wasijipe umalaika. Wanaotaka kuwa wanasiasa basi wavue haraka majoho na kupanda majukwaani. Serikali Yetu pia isisite kufuatilia mienendo ya baadhi ya viongozi wa Dini wenye kuonekana kuleta uchonganishi na kuchochea uhasama na chuki kwa watu dhidi ya serikali. Isikubali kuona kiongozi yeyote akifanya upotoshaji kwa watu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.