Viongozi wa dini mbona mmekaa kimya wakati CCM ikionyesha bango la ubaguzi Zanzibar?

Jan 1, 2016
80
12
Nimeshangazwa sana Na viongozi Wa dini zetu hapa Tanzania Kwa ukimya wao juu ya bango la ubaguzi lililoandaliwa Na CCM Na kupitishwa mbele ya viongozi mbalimbali Wa nchi hii Na mabalozi katika Uwanja Wa Amaan .

Viongozi hao wakati Wa uchaguzi mkuu Wa mwaka 2015 walimwandama Mh. Lowassa Wa Chadema kuwa alifanya kampeni kanisani lakini CCM mbele ya maelfu ya watu Na televisheni zilionyesha bango hilo dunia nzima bado viongozi hao wamekaa kimya kama vile bango hilo halina madhara.

Pia nazidi kuwashangaa viongozi hao kutokuwa sehemu ya usuluhishi wa mgogoro wa Zanzibar wakati waumini wao ndio wahusika. Kama kweli viongozi wa dini wanahubiri Amani, basi wakubali pia kuhubiri haki kwani haki isipopatikana basi na amani hutoweka.
 
Tanzania viongozi wa dini waliopo huwa muda wote wanazungumzia amani bila ta haki .wanaogopa wanapozunguzia kitu kuzungumzia haki .wanaogopa kuwaudhi watawala wa kidunia. Haki wanaijua ila wanaogopa
 
Sijui nani kawaloga hawa wanaojiita viongozi wa dini. Kweli watajibu mbele za Mungu. Kwa nini hawakemei uovu kwenye jamii?
 
Wamezimwa mdomo kwa kuambiwa wapeleke mahesabu ya misamaha ya kodi ya miaka 8 iliyopita wakati hao TRA na ukiwaambia tunaomba mapato na matumizi yenu tuu ya mwaka mmoja uliopita tuu watajikanyaga sana pamoja na pc zao zoote..
 
Chunga sana kuwasema viongozi hawa.....ukimya wao ni hekima tosha ukitaka waseme kila kitu hapatatosha
 
Kuna Baadhi ya members huku ni majipu. mojawapo Akiwa mleta uzi.
ccm walishaomba radhi kwa tukio Hilo siku ile ile limetokea. na ikawekwa huku ndani na Chachu Ombara. sasa viongozi wa dini waseme nini? au ndio kupenda ligi?
 
We vipi hapa tanzania kuna viongozi wa dini unadhani? Wote wale masheikh na maaskofu ni watumishi wa umma, wao wanangoja wakati wa kampeni wapite makanisani na misikitini kuhubiri amani, utawasikia watanzania msichezee amani utadhani wakati wa uchaguzi ni matatayalisho ya vita, hata siku moja sijawahi kuwasikia wakiubiri haki, au kukemea vitendo vinavyohatarisha amani,
Leo tumeona tulipoifikisha zanzibar, tumeshafanya chaguzi tano na zote matatizo ni yale yale yanajirudia lakini hakuna kiongozi yoyote anayesimama kukemea hadharani, wanachongoja damu imwagike alafu bila kumlaumu aliyesababisha haya, watajitokeza kwenye mikusanyiko ya watu na kujifanya wanaombea amani.
Hapa duniani kama unakaa na kuamini mienendo ya binadamu wenzio kisha wamejipa majina fulani na ukaacha kuamini na kutumia akili zako kutathmini mambo utapoteza sana muda hao ni viongozi wa dini wanatumiwa na wanasiasa kutokana na mahitaji yao mengi ya kimaisha.
Hivyo mtoa maada tafuta njia nzuri na mwafaka ya kudai na kuhakikisha haki yako inapatikana na kama ukingojea kwamba wachungaje na masheikh na maaskofu watakusemea utachelewa sana na mwisho utakata tamaa jambo ambalo mie sipendi likutokee,if you can,t beat them join them!
 
Back
Top Bottom