Viongozi wa dini Kiteto wafundwa..

Viongozi wa dini Kiteto wafundwa..

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya kiteto imewataka viongozi wa madhehebu ya kikristo kutekeleza wajibu wao wa ki-imani na kuepuka kuchanganya dini na siasa.

Wajumbe wa kamati hiyo wameeleza wajibu wa viongozi wa dini ni kutoa ushauri kwa hekima, kuliombea Taifa na viongozi wa serikali pamoja na kuwafundisha waumini kufanya kazi na kutii mamlaka za nchi.

Kamanda wa Uhamiaji Wilayani Kiteto Ikomba Eliud Mathew alisema, kuchanganya dini na siasa imekuwa chanzo cha kutoweka amani na utulivu katika mataifa mbalimbali na kuwataka viongozi hao, kusimamia msingi wa imani yao wa kutafuta amani na watu wote.

Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Kiteto Patrick Kimaro (Sabasita) amewakumbusha viongozi hao kuwa amani na utulivu vilivyopo ndio msingi wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali na kuwa, endapo amani itapotea hakuna shughuli yoyote ya maendeleo itafanyika ikiwemo kuhubiri neno la Mungu.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Kiteto Bw.Emmnuel Manyutwa amewakumbusha viongozi hao kuwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa kunachangia kupotea kwa amani na utulivu na kuzorotesha jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
 

Attachments

  • IMG-20180911-WA0044.jpg
    IMG-20180911-WA0044.jpg
    56.8 KB · Views: 19
  • IMG-20180911-WA0044.jpg
    IMG-20180911-WA0044.jpg
    56.8 KB · Views: 17
  • IMG-20180911-WA0046.jpg
    IMG-20180911-WA0046.jpg
    59.2 KB · Views: 18
  • IMG-20180911-WA0048.jpg
    IMG-20180911-WA0048.jpg
    65 KB · Views: 19
  • IMG-20180911-WA0041.jpg
    IMG-20180911-WA0041.jpg
    61.4 KB · Views: 21
Back
Top Bottom