Viongozi wa dini kemeeni kauli za vitisho za wanasiasa simamieni haki msiwe "biased"

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wadau wa JF,
Inavyoelekea baadhi ya viongozi wa dini wameanza kuonyesha dalili au kutekwa na siasa, viongozi wa dini ndiyo muhimili mkubwa kutokana na hadhi yao mbele ya jamii yetu ya kitanzania.

Viongozi wa dini wameamua kukemea maovu yanayofanywa na watu fulani kwa wakati fulani na kuacha kukemea maovu ya aina hiyo yapofanywa na wengine ebu angalia ujumbe huu kutoka kwa kiongozi wa kisiasa.

"Nasubiri simu yako wajulishe polisi wako waandae risasi za moto mtakakuwa na karamu kusherekea mauaji, na mjiandae kwa kwenda mahakama ya The Hague, ni afadhali kufa kuliko manyanyaso haya"

Kauli kama hii viongozi wa dini hawajatendea haki kwa waumini wao wamekaa kimya kama vile hii kauli aina madhara, na hatimaye raia wamepoteza maisha kwa vifo.
 
Back
Top Bottom