Katika kampeni za CCM huko Igunga sijasikia viongozi wa chama hicho wanaongelea masuala yanayoiunguza taifa kutopiga hatua mbele -- ufisadi, ukosefu wa umeme etc. Kwa nini wanapata kigugumizi kikubwa kuyaongelea haya? Wanaogopa nini? Wanaogopa kwa sababu wengi wa viongozi wa CCM siyo wasafi kabisa. Sauti haziwezi kutoka mdomoni wakiwa majukwaani wanapotaka kutaja neno 'UFISADI.'
Kukosekana kuzungumzia ufisadi wana-Igunga wanawashangaa sana.
Nawapa hongera CDM kwa kuongelea bila wasiwasi suala la ufisadi -- wameonyesha ujasiri mkubwa.