Viongozi wa CCM wanaogopa kuzumgumzia ufisadi katika kampeni zao Igunga

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Katika kampeni za CCM huko Igunga sijasikia viongozi wa chama hicho wanaongelea masuala yanayoiunguza taifa kutopiga hatua mbele -- ufisadi, ukosefu wa umeme etc. Kwa nini wanapata kigugumizi kikubwa kuyaongelea haya? Wanaogopa nini? Wanaogopa kwa sababu wengi wa viongozi wa CCM siyo wasafi kabisa. Sauti haziwezi kutoka mdomoni wakiwa majukwaani wanapotaka kutaja neno 'UFISADI.'

Kukosekana kuzungumzia ufisadi wana-Igunga wanawashangaa sana.

Nawapa hongera CDM kwa kuongelea bila wasiwasi suala la ufisadi -- wameonyesha ujasiri mkubwa.
 
Mkuu, kama unavyosema sauti haziwezi kutoka. Wanachoweza ni kupanga watu kupiga gari zao mawe au kumwagia tindikali na halafu kuomba huruma ya polisi. Kwao ufiswadi si tatizo, lakini vitambi vyao vinawasuta saana, maana havijifichi.
 
Mwalimu wangu wa philosophy aliwahi kusema hivi " A politician is able to do anything to achieve his goals ". Ndio kinachotokea Igunga leo,
 
Weee...wanamuogopa Rostam. Fisadi namba 1 ni Rostam, halafu waseme fyeee huko Igunga kama hawatatoka kapa. Rostam bado ni muhimili wa CCM hawawezi wakasema chochote cha kumuudhi huko Igunga. Hata yule Nepi wao hawezi ropoka hata kidogo....hao ndi CCM a.k.a Magamba a.k.a Chama Cha Mafisadi.
 
Mkuu,
Majibu ni so obvious! Kwa binadamu ni vigumu kuzungumzia mapungufu yake hadharani. Sote tunajua kuwa mafisadi wote ni ccm. Kwakuwa wananchi ( wakiwemo wa Igunga ) wanakerwa na kuumizwa na ufisadi, midomo yao inashindwa kuongea yasiyotoka moyoni! Na kwakuwa wananchi wameshajua, sasa hukumu yao inaanzia Igunga!
 
Back
Top Bottom