GE2025 Viongozi wa CCM Geita walalamikia kukithiri kwa rushwa kura za maoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Geita Mjini mkoani Geita wameeleza kusikitishwa kwao na namna mchakato wa kura za maoni za kupata wagombea ubunge na madiwani ulivyokwenda huku wakidai kugubikwa na rushwa kwa baadhi wagombea na wajumbe.

Wakizungumza na JAMBO TV kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho wamedai baadhi ya watia nia walionekana wakitoa rushwa ya fedha na vitenge kwa wajumbe hali ambayo imeibua wasiwasi juu ya uhalali wa wagombea hao huku wakiomba viongozi ngazi za juu kuingilia kati.

Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita, Michael Msuya mbali na kutotaka kuzungumzia suala hilo amedai chama kina utaratibu wake hivyo mwenye malalamiko awasilishe.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, James Ruge akizungumza kwa njia ya Simu na JAMBO TV amekiri kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi huku akiahidi kutoa taarifa kamili Agosti 13, 2025.

Your browser is not able to display this video.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…