Viongozi wa CCM acheni unafiki kwa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CCM acheni unafiki kwa JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fiksiman, Apr 11, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi karibu Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga wamepitisha azimio la kutomtambua mgombea yeyote atayejitokeza kupambana na Rais Kikwete uchaguzi ujao ndani ya chama chao. Kauli hii pia naweza kusema kuwa inapigiwa debe na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho John Malecela. Huu ni unafiki mkubwa tena wanatuonyesha jinsi gani walivyo miamba ya kukiuka si tu katiba yao hata Ile ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

  Ikumbukwe kuwa kwa CCM jambo kubwa na msingi sasa si kanuni na katiba bali utamaduni...hakuna sehemu iliyoandikwa kuwa Rais aachiwe miaka kumi ila ni utaratibu wa kawaida ambao inatokana na busara ya wanachama wenyewe...na huwezi kumlazimisha mtu kuwa na busara. Pia hata kama hutaki kweli si muumsubiri ulingoni aadhirike basi kwa shida iko wapi kama kweli mnamkubali huyo Rais wenu (Kuna ajenda gani hapa viongozi hawa wanakwepa kuionyesha??)..isije kuwa hadithi ya bwana mbuni kufunika kichwa huku kiwiliwili chote kiko nje akiamini hawezi kuonekana na maadui zake.

  Mi nilidhani CCM itakuwa imesoma alama za nyakati na kumpa changamoto Rais wao aweze kujiandaa vyema na kitakachotokea mbeleni. Kama kweli wanatoa kipaumbele suala la utamaduni mbona waligoma kuwaachia wazanzibar mwaka 2005 kutoa mgombea??? Tena wakasema waziwazi kuwa hakuna suala hilo la awamu hii BARA na ile Zanzibar! Tuache unafiki na wala hamumsaidii Rais Kikwete, tena nahisi mnataka aadhirike kwani akianguka kwa wanachi mseme mlijaribu kumbeba yeye mwenyewe habebeki.

  Sasa mi nataka kuwashauri jambo moja kubwa: Kikwete hadi sasa ana hali mbaya kisiasa na bila kumpa mpinzani ndani ya chama chenu basi mjue mko mguu ndani mguu nje. Mnaweza kujipa matumaini kwa kuwa watu hawasemi sana juu yake ni dalili njema mujue tu watanzania tunajua kinachoendelea sasa kwahiyo majibu mtayapata na ole wenu mkiteleza kama mnavyofanya sasa.

  "kama hamtapa mpinzani nyumbani kwenu basi uwanjani atapewa"
   
Loading...