Viongozi wa Afrika na story ya udereva (fumbo na mtazamo)

GENIUS JAGUAR MONSTER

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
257
250
Wazo

Tanzania ni kama gari na rais ni dereva. Na Watanzania ni abiria. Lakini gari lilianzwa kuendeshwa na mzungu kwenye uelekeo waliokua wanaujua wao kwa mda mrefu sana. Walichokijadili kuhusu mwelekeo wa gari kilikua ni siri. Lakini wakaona kuendesha gari huku abiria waliomo hawampendi dereva itakua kazi. Wakajadili kwa siri wakaweka mipango alafu...

Mara ghafla vuuup! Akaachiwa gari nyarere lakini likiwa katika speed kali. Na abiria waliomo wote wakaaminishwa na Nyerere sasa tunaenda kwenye mwelekeo sahihi huku Nyerere akijaribu kutafuta njia sahihi kwa abiria wake. Akasahau kwamba waliomfundisha gari ni hao hao wazungu. Na standard nzuri za kuendesha gari waliziweka wao na system ya gari waliiweka wao na hata wakitaka kulipua gari wanaweza maana wao ndo wana remote ya kila sehemu ya gari.

Basi kumbe ujanja ilikua ni kutoka kabisa kwenye lile gari na kushusha abiria wake na kutengeneza gari lake na kutafuta muelekeo mwingine.

Nyerere alikuja kushtuka tunatakiwa tutoke ndani ya gari mda umeenda. Basi akamuachia majukumu Mwinyi

Inaendelea

Basi Mwinyi alivolishika lile gari ndo kwanza akaweka wazungu kua makonda na madereva wasaidizi. Na spare zote za gari akawa anatoa kwao. Basi wazungu wakawa hawana shida na mwanyi kwa sababu gari bado inakimbia kwenye muelekeo wanaoutaka.

Akaja Mkapa. Akawa mkali na kutoa elimu jinsi ya kuendesha gari alilotengeneza mzungu na kuelekea muelekeo ule ule. Hakuna kilichobadilika na alichoki dream nyarere kikazidi kufifia. Abiria wanazidi kuelimishwa kuhusu gari ya mzungu na kuelekea muelekeo wa mzungu.

Basi akaingia JK. Huyu. Alipeleka gari katika muelekeo ule ule na kuzidi kuimalisha elimu ya gari ya mzungu na muelekeo wake. Hadi abiria wa kizungu wakaanza kuingia kwenye gari na kuwatoa abiria Watanzania kwenye siti zao na kuwekwa kwenye siti nzuri kabisa.


Lengo likawa abiria wote wa kizungu wakae na abiria wote wa kitanzania wasimame. Kwa sababu magari ya wazungu huko ulaya yote yamejaa. So ni bora kutafuta magari kwenye nchi za africa na kuwatoa waafrica kwenye siti zao.

Ikaenda ikawa mazoea. Mara ghafla vuuuuuuuuup. Akaingia muheshimiwa "m". Huyu muheshimiwa yeye alikua ana madhumuni makubwa sana ya kuondoa ghali kwenye muelekeo. Ila alivofika kwenye gari kama dereva. Akaona kubadili muelekeo wa gari kunahitajika umoja wa madereva wote africa ili kubadili muelekeo na kutoka kwenye magari. Japokua ana pambana na umoja ikashindikana.

Story ya dereva wa Libya
Huyu dereva (Gadafi) alikua anania na uwezo na maono ya kutoka kwenye gari na kutengeneza gari moja ya waafrika na kuchagua muelekeo wanaoutaka. Ila watengeneza gari walivostuka. Walimuondoa fasta kwa sababu gari zote Africa zisipoelekea mwelekeo aliouweka mzungu basi wenda madereva na abiria wa kizungu wanaweza kua kwenye wakati mgumu sana.

Basi ni hayo tu wakuu. Ila najua mumeona picha kubwa sasa.

Ni mtazamo tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom