Viongozi tuwe na busara, tusitumie sheria kukomoana! Ipo kesho tuifikirie

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Viongozi wengi wamekua wakinyanyasa sana watu hasa awamu hii ya tano, wamekua wakisingizia kua "NAFUATA SHERIA" ili kuhalalisha uonevu wao. Ikumbukwe hata hizi sheria zimetungwa na wanadamu sio malaika wala Mungu au manabii wake.Busara na hekima ni kitu muhimu sana katika kutekeleza majukumu yetu maana kesho nayo ipo wakati tutakapokua tumewaachi vyeo hawa tunaowaonea leo.


Hata vitabu vya Mungu vinasema kua "akukoseaye msamehe saba mara sabini" na "Auaye kwa upanga naye huuawa kwa upanga". Hii misemo ni mizito mno kwa watu wenye akili timamu na wenye hofu ya Mungu.

Unaninyanyasa mimi leo, cheo ni dhamana! haupo kesho wewe atakuwepo mwanao, nitatumia na mimi sheria hii hii kukuadabisha na wewe na ikiwezekana nitachomekea na visasi zaidi. Kwahiyo utu ni muhimu sana sana kwetu sisi maana dunia ni mviringo.


Hata mahakamani pamoja na mkusanyiko wa nyaraka nyingi za ushahidi juu ya kosa alotenda mtuhumiwa, lakini bado mahakama huangalia na hali halisi pamoja na utu.Tusiwe wa sahaulifu tutembee na bwana! tuache vitendo vya kinyama maofisini kwa kusingizia kua unafuata sheria.
 
Back
Top Bottom