Viongozi Tanzania wanakera

Viongozi Tanzania wanakera

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
394
Reaction score
627
Ndugu Watanzania,
Nimemsikiliza Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Kayanza Piter Pinda kwenye hotuba yake leo akiwa bungeni sikuamini kuwa na yeye amekuwa sio mototo wa Mkulima tena bali Fisadi na Mtetea maovu ndani ya chama Tawala. Naweza kusema Pumu imepata Kikohozi. Waziri Mkuu ameonyeshwa kukerwa na watu wanaoipinga Serekali dhalimu ya CCM lakini hakerwi na Mawaziri na Watendaji ndani ya Serekali yake wanaoiba kodi za Watanzania.

Kwa kauli yake amesema watu wanaokusanyika bila vibali na kukaidi kauli za Jeshi la Polisi hata kama hazijatolewa wapate mkon’goto. Mimi nikajiuliza kwa hiyo hata tukiwa kwenye mikusanyiko ya makanisani, misikitini, kuzika wapendwa wetu tupigwe mikongoto kwa kuwa Waziri Mkuu katoa maagizo. Hivi ikiwa hivi nchi itakuwaje?. Kwa maana hiyo kelele za Watanzania kuwa ashuhulikie ufisadi na hafanyi hivyo na sisi tumpige mikon’goto kwenye misafara yake. Cheo ni dhamana tu. Watanzania wanayo haki ya kuihoji Serekali. Kule Arusha Polisi wamepiga watu bila sababu na kuiba mali za watu ikiwa ni pamoja na kuvunja magari vioo na kuiba Redio na mali zingine zilizokuwemo ndani. Ndio maana nasema nchi haitatawalika.

Kama Waziri Mkuu anachukia mikusanyiko lakini anafurahia Ufisadi na Watanzania kupigwa na vyombo vya dola haya ni Maajabu. Waziri Mkuu anakuwa mkali kukemea mikusanyiko lakini anakuwa mpole kukemea ufisadi na Wizi wa mali za umma ni hatari. Waziri mkuu anatembelea wagonjwa waliopigwa mabomu wakiwemo watoto wasio na hatia na Jeshi lake la Polisi kwa makusudi na kutoa pole kinafiki, alafu anajisahau alikuwa Hospitali arudi aseme Piga wakileta kiburi ni hatari sana. Anauma na kupuliza. Viongozi wa Tanzania wanatumia sasa hivi jeshi la wajinga Polisi kuhakikisha yafuatayo.

-Kuhakikisha wanapora mali za Watanzania zikiwemo nyara za wanyama kama Pembe za Tembo na mali zingine walizozalisha Watanzania na kuzifanya za familia zao tukidai watembeze mkon’goto hii ni hatari.

-Kuhakikisha wanatoa elimu mbovu isiyokidhi wala isiyomsaidia mtoto wa masikini Tanzania tukidai waboresha elimu watupige risasi na mabomu hii ni hatari.

-Kuhakikisha inabariki rushwa rohoni lakini mdomoni wanapiga vita na kukemea tukihoji kwa nini wanaruhusu rushwa tupigwe na mabomu na risasi za moto.

-Kuhakikisha inawaua waandishi wote wenye kutaka kuvuruga utawala wao wa kifisadi tukihoji tunapigwa mabomu, kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa risasi na mabomu.

-Kuhakikisha Demokrasia Tanzania haipati nafasi kabisa kwa kuwaweka ndani viongozi wa vyama vya siasa na kuwafungulia kesi za ugaidi wa kutumia Jeshi la Polisi.

-Kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinanufaisha watoto wao tu kwa hivyo hakuna mtu hata mmoja anaona mikataba ya Wawekezaji awe Mbunge wa chama cha Siasa au Raia wa Tanzania.

-Kuhakikisha wanawagawa Watanzania kwa imani za kidini waendelee kutawala Tanzania na Serekali dhalimu ya CCM na Jeshi la Polisi.

-Kuhakikisha wanawagawa Watanzania kwa imani za Kikabila waendelee kutawala Tanzania na Serekali dhalimu ya CCM na Jeshi la Polisi.

-Kuhakikisha wanawagawa Watanzania Kikanda waendelee kutawala Tanzania na Serekali dhalimu ya CCM na Jeshi la Polisi.

-Kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa fedha chafu ziwasaidie kwenye chaguzi mbali mbali Tanzania.
-Kuhakikisha kila muwekezaji anayewekeza Tanzania anaigia kwenye mfumo wao wa Kifisadi.

-Kuhakikisha Rais wa Tanzania anapatikana kwenye mfumo wao rushwa na Ufisadi.

-Kuhakikisha kila Wizara inakuwa na kijana wao anayetokana na mtandao wao wa rushwa na Ufisadi.

-Kuhakikisha biashara zote kubwa kubwa ni mali yao kwa kuinyima Serekali kusimamia viwanda vyake vya uzalishaji.

-Kuhakikisha wanaua na kuwajeruhi Watanzania mahali popote penye mikusanyiko ya vyama vya Siasa ili kuwatia hofu ya kujiunga na vyama vya upinzani kudai haki zao.

-Kuhakikisha biashara zote za uagizaji bidhaa nje wanafanya wao kwa kuua viwanda vyote vya ndani kwa kisingizio kuwa Serekali haitaki kufanya biashara.

-Kuhakikisha Watanzania wanazidi kuwa wajinga wasijue mapato na matumizi ya Serekali yao ndio maana hakuna mitaala ya shule ya kuelewekaq, na wakaua elimu ya watu wazima.

-Kuhakikisha elimu ya uraia haitolewi mashuleni nchini Tanzania ili wasijue Mtandao wa utawala wa CCM una malengo gani.

-Kuhakikisha madini na rasilimali za nchi hii zinawanufaisha wao tu na watoto wao na kujilimbikizia masli nje ya nchi.


TUFANYE NINI WATANZANIA
-Lazima tuwe na mshikamano bila kujali Itikadi zetu za vyama, Dini zetu, kabila zetu, jinsia zetu na rangi zetu kuhakikisha haturuhusu Mtandao wa Mafisadi wa chama tawala CCM kufanya Tanzania ni koloni lao au wamekatia hati miliki. Chukua fedha zao na piga kimya kimya kwenye chama cha upinzani maana hii ni kama unarudishiwa sehemu ya kodi yako waliyokwapua.

-Lazima kuishitaki Serekali nzima ya CCM na washirika wake kwenye Mahakama ya Kimataifa ICC kwa kuwaua Watanzania wenye ulemavu na wasio walemavu zaidi ya 130 bila hatia yoyote, Kuwekeza bila kuweka bayana mikataba ya uwekezaji, na kuvunja Makazi ya watu bila fidia kwa ajili ya kuweka wawekezaji.

-Lazima kuishitaki Serekali nzima ya CCM na washirika wake kwa kuendekeza rushwa na kuficha kiasi kikubwa cha fedha nje ya nchi huku wakifanya biashara za madawa ya kulevya.

-Lazima kuishitaki Serekali ya CCM na washirika wake kwa kuua viwanda na mashirika ya umma na kujiuzia mali za Taifa kwa bei za kutupa. Angalia ulikotoka, au uklikozaliwa watu wanavyotaabika. Watanzania tuko tayari kutoa ushahidi kama Waliberia walivyotoa ushahidi kwa CHARLES TAYLOR.

Waswahili walisema ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni anaweza fanana na ndugu yako, mjomba wako, au vinginevyo. Watanzania tusitumiwe vibaya na Serekali ya CCM katika Dini zetu, Kabila zetu ili kuendelea kuwaweka madarakani. Jiulize watu wana mabilioni wameficha ulaya, majumba ya kifahari, magari ya kifahari, mashamba, viwanda, makampuni je wewe Mmatengo, Msukuma, Mhaya, Mmakua, Mkerewe, Mdigo, Mzaramo, Mrangi, Mmbulu, Mmatumbi, Mpogoro, Mdengereko, Mchagga, Mpare, Msambaa, Mmwera, Mnyiramba, Mnyaturu, Muikizu, Mjita, Mha, Mholoholo, Mvinza, na wengine wengi kama mimi Mhaya tuna nini wametuwekezea CCM kwa ajili ya watoto wetu na wajukuu zetu kwa miaka 50. Mbaya kabisa wanamtania mtani wangu wanamwambia ukitaka mzigo ufike mpe Mnyamwezi.

Hivi kweli Watanzania tumekosa kabisa mtu wetu muaminifu kama Mwalimu Julius Kambara Nyerere wa kumuweka Ikulu. Hebu tuache itikadi za vyama, udini, ukabila, ukanda, tufanye maamuzi sahihi. Dunia inatucheka, majirani zetu wanatucheka kwa utajiri tulio nao lakini hatuna mikakati ya kuondoa Umasikini, Ujinga na Maradhi. Rwanda wamepigana vita leo hii wana mandege yanakuja mpaka Tanzania. Kuanzia sasa mgeukie mwenzako alieko karibu nawe na mwambie acha itikadi za vyama, acha Udini, acha ukabila, acha ukanda, acha kukumbatia rushwa na mafisadi wa CCM. Watanzania kwa pamoja tunaweza kuifanya Tanzania ikazaliwa upya. Nchi imeoza kwa utawala wa Kifisadi. Nchi imeharibika kwa kupigwa hovyo na Polisi. Hivi mtoto wako akila chakula bila ridhaa yako mbona unamkanya. Mbona ndani ya CCM Wizi, rushwa, ubadhirifu, unyang’anyi, mauaji, uporaji, uhamishaji fedha za umma, udhalimu, vimetawala lakini mwenyekiti wao yuko kimya. Watanzania Tuchukueni tahadhari.
“TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA”​
Mkereketwa

LENGAI OLE LETIPIPI
 
Kiongozi bora hawezi kupatikana tena CCM.Mwalimu katika hili ali overlook kidogo.Leo hii kiongozi mbovu hawezi kupatikana nje ya CCM.
 
Back
Top Bottom