Viongozi na umiliki wa silaha.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi na umiliki wa silaha....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Davie, Sep 1, 2012.

 1. D

  Davie Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Imekuwa ni kawaida sasa hivi kwa watu mbalimbali kumiliki silaha hapa nchini..na wengi wao wanadai ni kwa ajili ya ulinzi wao binafsi na mali zao. Na hiyo ni mojawapo ya vigezo vya mwananchi wa kawaida kumiliki silaha..

  Lakini hivi karibuni imetolewa taarifa ya baadhi ya wana CCM wakitishiana silaha hizo za moto kwenye kinyanganyiro cha uongozi wa CCM huko wilayani Nzega..

  Suala linalonipa shida ni kwanini viongozi wanamiliki silaha na tena wanazitumia vibaya.... Je hawajui sheria za matumizi ya hizo silaha za moto.... Ukifuatilia matukio utajua nini nakizungumzia..

  1. Rage alionyesha kwa makusudi silaha yake kwenye mkutano wa kampeni huko Igunga na polisi wakamhoji..na sijui liliishia wapi..
  2. Hawa Bashe na Kigwangalla..nao kama kawaida wametoleana bastola hadharani..
  3. Malima nae alikuwa na bastola na SMG..ingawa la SMG ni vigumu maana ni ya kijeshi..
  4. Marehemu Ditopile alimtolea bastola dereva daladala....."akawa anamgongea dirishani dereva wa daladala ili afungue..bahati mbaya ikajifyatua yenyewe".....

  swali langu ni je...inamaana umiliki wa silaha sasa ivi umebadilika...ama ndo kwakuwa ni wanatokea chama tawala..ama ndo ulimbukeni...
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa kuleta hii hoja mezani. Tatizo la silaha mitaani ni tishio kubwa sana. Viongozi wengi wakiwemo wabunge (vyama vyote) wanamiliki silaha. Na sababu kubwa ni udhaifu wa jeshi la polisi kulinda usalama wa raia na mali zake, badala yake sasa polisi wameona njia rahisi ni kuruhusu mtu mmoja mmoja kumiliki silaha - self defense!

  Kuna haja kabisa ya kuangalia upya hili jambo kabla hatugeuza Tanzania ikawa kama Marekani. Mtu kama Adam Malima anasifiri na SMG! Adam Rage anahutubia wakina mama na watoto huku bastola ikining'inia kiunonu mwake mchana kweupe?

  Kama uongozi wa polisi na serikali ya CCM wameshindwa kuangalia uraia bila silaha (kama ilivyokuwa zamani) hakuna haja ya kuendelea na hao watu. Solution haiwezi kugawa silaha kama njugu, hii ni hatari kubwa na ningefurahi wananchi wanapaza sauti.
   
 3. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  serikali izue viongozi wa kisiasa kuwa na slaa, coz cjawahi kusikia aliyejeruhiwa au aliyeshambuliwa na kuitumia hiyo slaa...
   
Loading...