Viongozi na mawaziri wengi wanatakiwa kuachia ngazi kutokana na kauli zao

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
147
Ndugu wana JF,

Nimekuwa nikitafakari jinsi ambavyo aliyekuwa Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Ms Susan Rice, alivyonyimwa nafasi ya kuwa Secretary of the State (Waziri wa mambo ya nje) hata baada ya jina lake kupendekezwa na Rais Obama. Kilichomponza Susan Rice ni TAMKO ALILOTOA KUHUSU KUVAMIWA KWA UBALOZI WA MAREKANI MJINI BENGHAZI - LIBYA. Maelezo aliyoyatoa hayakuwa sahihi. Japokuwa alijitetea kwa kusema yeye alitaarifiwa hivyo, hata hivyo alipoteza sifa ya kuwa Secretary of State.

Sasa narejea kwenye matamko mengi ambayo yamekua yakitolewa na viongozi wetu, zaidi sana Mawaziri na viongozi wa vyama​. Wengi wamekuwa wakitoa matamko ambayo ama yanapingana na msimamo wa Rais au yasio na ukweli. Hata hivyo watu hawa bado huachwa na kuendelea na kazi pasipo kuwajibishwa kwa kauli zao.

Nitoe mifano michache; ila naamini wana JF mtakuwa na mifano mingi zaidi:

1. Tamko la Mh. Samuel Sitta kuhusu afya ya Dr. Mwakyembe. Alitamka waziwazi akiwa pamoja na viongozi wengine ya kwamba Dr. Mwakyembe kalishwa sumu na kwamba anawajua walomtendea hivyo. Hili tamko lilihitaji mtu awajibishwe.

2. Tamko la Mh. Wasira kwamba Wapinzani hawatakua na nafasi tena ya kwenda Ikulu kumuona Rais kwa swala la katiba. Akaendelea kusema wanataka kwenda Ikulu kunywa chai na juice. Lakini tumeshuhudia Mh. Rais akiwaita viongozi wa upinzani Ikulu kujadili mstakabali wa Taifa letu. Je, Mh. Wasira hapaswi kuwajibishwa?

3. Jana nimesoma taarifa kwamba Mh. Sofia Simba anadai CHADEMA inatumiwa na Mataifa ya nje kuvuruga nchi. Je hilo lisipothibitishwa, atawajibika?

4. Mh. Waziri Mkuu, ndugu Pinda kwa kutoa kauli ya kusema, "Tumechoka...Wapigeni tuu..." Ni kweli inawezekana alikuwa ameghafilika; lakini si ingekuwa busara kwa yeye kufuta kauli yake na kuwaomba wananchi msamaha?

5. Mh. Lipumba, Mwenyekiti wa CUF alinukuliwa akisema walitumia kigezo cha UDINI ili kumsaidia Mh. Rais katika uchaguzi. Ningetazamia Ikulu itoe tamko kupinga hilo na pia Mh. Lipumba ingepaswa awajibike!!

Ni wakati sasa kwa viongozi wetu kujifunza kuwa waangalifu na maneno wanayoyatamka. Na pale ambapo wanakuwa wametoa kauli za upotoshaji basi ni vyema tuanze utamaduni wa kuwawajibisha viongozi kwa kauli zao.
 
Back
Top Bottom