Viongozi Madikteta na kauli mbiu yao ya kulinda rasilimali

Viongozi Madikteta na kauli mbiu yao ya kulinda rasilimali

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,377
Reaction score
4,847
Dikteta ni nini/nani. ni mfumo ambapo kikundi cha watu wachache au mmoja wanatawala nchi kwa mtutu, wakiwa juu ya sheria, wakiua watawaliwa, kuteka, kubaka na hata kunyanganya mali za watu.

Sifa kuu ya madikteta ni kuvishika na kuvitawala vyombo vya ulinzi na Usalama.

Kwa nyakati za hivi karibuni limeibuka wimbi la Madikteta katili duniani jinsia zote wa kiume na wakike wakitawala kwa mtutu na bunduki na mikono yenye kunuka damu.

Hawa Jamaa wamegundua Slogan yao WANALINDA RASILIMALI ZA NCHI, wanatumia Slogan hiyo kuhalalisha uharamia wao.

Wanamiliki magenge ambayo huteka watu na hata kuua kwa mlengo wa kuwalinda madikteta.

Mbaya zaidi kuna watawaliwa nao kazi yao imekua kuwasifu madikteta wakidanganywa na vipande 30 vya fedha huku maisha yao yakizidi kuwa magumu siku baada ya siku.

Watawala waovu waache kujificha kwenye kivuli cha kulinda rasirimali.
 
Kila dikteta duniani kakariri hii sentensi na anaitumia vilivyo kuua ndugu zake
 
Tanzania hili lipo sana.Ndo kificho wanachojifichia.Wakati hata sasa rasilimali hizo zinachotwa sana tu
 
Mmelishwa sumu na kulilishwa uongo wa demokrasia ya kimarekani inayotenda kazi nyuma ya kapeti.
 
Rasilimali gani washenzi tu wale, mbona US, UK inalinda rasilimali na haki za wengine?
 
Mmelishwa sumu na kulilishwa uongo wa demokrasia ya kimarekani inayotenda kazi nyuma ya kapeti.
Rais wako kashinda kwa asilimia ngapi, wewe Ges ya Mtwara unaifaidi vipi, Chuma, makaa ya mawe huku ukizidi kuishi kwenye umaskini wa kutupwa, Marekani ana demokrasia kweli na Kiboko ya madikteta uchwara.
 
Back
Top Bottom