Nilikuwa nasikiliza maelezo ya Viongozi wetu wa Taifa kwa wateuliwa wa Rais baada ya kula kiapo cha kazi zao. Moja ya mambo yaliyonishangaza ni pale Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai aliposimama na kuwaasa majaji kuwa ni muhimu kwao kutenda haki pale wanapotoa maamuzi ya kesi watakazokwenda kuzisikiliza
Huo ulikuwa ni ushauri murua kabisa, tatizo kwangu likaja pale nilipokuwa natafakari juu ya maamuzi ambayo spika huyu wa Bunge letu amekuwa ameyafanya huko bungeni kama yanasahabihiana na ushauri alikuwa anawapa hao majaji?
Hebu tuchunguze moja ya maamuzi ambayo Spika Ndugai ameyatoa hapo bungeni hivi karibuni nalo ni lile linalohusu wabunge waliofukuzwa na chama chao kuruhusiwa kuendelea kuwa Bungeni. Katiba inatamka wazi kabisa kuwa mwananchi yeyote hawezi kuwa mbunge kama sio mwanachama wa chama cha Siasa. Hivyo kwa kuwakubalia wale wakina mama waliofukzwa na Chadema kuendelea kuwa Bungeni Ndugai anavunja katiba na hivyo hatendi haki. Kutenda haki maana yake ni kuheshimu na kulinda sheria za nchi!!
Kwanini Ndugai anavunja sheria ya nchi na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa? Yote hii inatokana na TAASISI yetu ya Bunge kuwa DHAIFU. Kama Bunge letu lingekuwa imara , lingekuwa linaongozwa na Katiba na sheria ambazo Bunge hilo hilo limeapa kulinda na kutetea hayo yote yasingetokea na haki ingetendeka! Hivyo basi ili kuwa na Taasisi imara ni wazi kuwa Katiba iliyokubaliwa na wananchi ni lazima iheshimiwe.
OUR LEADERS MUST WALK THE TALK!!