Mleta Thread uko sahihi,ndiyo maana nilishawahi kusema humu JF pia kama kweli JPM anamalengo ya dhati ya kuwakomboa Watz. suala lakwanza kulifanya ni Kupata Katiba ya Mpya Wanachi iliyosimamiwa na Tume ya Jaji Warioba na kuiboresha zaidi na siyo vinginevyo.
Kupitia mtego ambao ninaweza sema uliondaliwa na CHADEMA wa operesheni UKUTA wananchi wengi tumegundua mambo mengi sana kuanzia Serikali,Sekta za Umma,Taasisi na vyombo vyote vya Dola ambavyo hatukutegemea kama navyo viko kisiasa.
Hata akiingia kiongozi gani yeyote yule wa chama chochote kile kwa upande wangu ninasema ni Zero kama HAKUNA Katiba mpya.
Haiwezekani Wateule wa Rais wakafanya au kutenda Jambo tofauti na Mteuzi wao anavyotaka,wengi tumewaona wanavyo vunja Katiba na Sheria za nchi.
Hatuwezi fika popote pale pasipo Katiba Mpya isiyo mlinda yeyote yule atakaye vunja sheria ilimradi yuko chini ya jua hili.
Mfano Tumeona Rais wa Brazili yuko nje ya Ikulu sasa kwa kufuja mali za nchi,tunataka kila mmoja awajibike kwa nafasi yake na siyo wako walio juu ya Katiba nchi hii ni ya maajabu kwelikweli yaliyo nje sayari ya Tatu.
Mfano.Mamlaka ya Rais yanatakiwa yapunguzwe kwani yamepitiliza na kadha wa kadha.
Acha niishie hapa tu maana kuna wakati ninapata hasira kweli hasa ninapoona,kusikia na kutafakari Nchi yangu ya kusadikika mambo yanyoendelea na kutokea.