Ili kuongeza tija na ufanisi kwa watendaji wakubwa serikalini ni vyema bunge lipewe mamlaka ya kuwajadili na kuwaidhinisha watendaji wakubwa serikalini. Viongozi wanaopaswa kujadiliwa kwa kina :
1. Mawaziri
2. Mkuu wa majeshi
3. Mkuu wa jeshi la polisi
4. Majaji wa mahakama kuu/ Rufaa
5. Wakuu wa Mikoa
7. Mabalozi
8. Wakuu wa taasisi mbali mbali za Kiserikali.
Hii itasaidi kupunguza viongozi wa kiserikali kuwa makada wa kisiasa, upo udhaifu mkubwa kwa watendaji wengi serikalini si kwamba hawana sifa bali wapo kwa maslahi ya kiongozi aliyewaweka madarakani. Viongozi hawa badala ya kulinda maslahi ya taifa wamegeuka watetezi wakubwa wa madhambi, kitendo cha mkurugenzi mkuu Tukukuru kudai Chenge hahusiki na kashfa ya rada ni mmoja tu mfano hai. Mfumo huu si tu utaongeza ufanisi bali utasaidia viongozi hao kuwajibika kwa wananchi badala ya Raisi aliyewaweka madarakani.
Ni vyema wabunge wetu wakiliangalia hili kwa makini zaidi, ni hatari sana kwa mtu kama mkuu wa jeshi kujihisisha na siasa badala kuangalia ulinzi wa taifa letu. Ama vitendo vya majaji kugeuka makada badala ya kulinda sheria.