Viongozi hao wajadiliwe na Bunge kabla ya kushika nafasi zao.

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,418
Ili kuongeza tija na ufanisi kwa watendaji wakubwa serikalini ni vyema bunge lipewe mamlaka ya kuwajadili na kuwaidhinisha watendaji wakubwa serikalini. Viongozi wanaopaswa kujadiliwa kwa kina :
1. Mawaziri
2. Mkuu wa majeshi
3. Mkuu wa jeshi la polisi
4. Majaji wa mahakama kuu/ Rufaa
5. Wakuu wa Mikoa
7. Mabalozi
8. Wakuu wa taasisi mbali mbali za Kiserikali.
Hii itasaidi kupunguza viongozi wa kiserikali kuwa makada wa kisiasa, upo udhaifu mkubwa kwa watendaji wengi serikalini si kwamba hawana sifa bali wapo kwa maslahi ya kiongozi aliyewaweka madarakani. Viongozi hawa badala ya kulinda maslahi ya taifa wamegeuka watetezi wakubwa wa madhambi, kitendo cha mkurugenzi mkuu Tukukuru kudai Chenge hahusiki na kashfa ya rada ni mmoja tu mfano hai. Mfumo huu si tu utaongeza ufanisi bali utasaidia viongozi hao kuwajibika kwa wananchi badala ya Raisi aliyewaweka madarakani.
Ni vyema wabunge wetu wakiliangalia hili kwa makini zaidi, ni hatari sana kwa mtu kama mkuu wa jeshi kujihisisha na siasa badala kuangalia ulinzi wa taifa letu. Ama vitendo vya majaji kugeuka makada badala ya kulinda sheria.
 
vetting pannel
muhimu sana, inapaswa rais apendekeze jina kisha vetting pannel iwe inathibitisha kuondoa upendeleo, pia itasaidia kupata kiongozi bora sio bora kiongozi.

sheria na katiba zinahitaji mabadiliko...
 
Mleta Thread uko sahihi,ndiyo maana nilishawahi kusema humu JF pia kama kweli JPM anamalengo ya dhati ya kuwakomboa Watz. suala lakwanza kulifanya ni Kupata Katiba ya Mpya Wanachi iliyosimamiwa na Tume ya Jaji Warioba na kuiboresha zaidi na siyo vinginevyo.
Kupitia mtego ambao ninaweza sema uliondaliwa na CHADEMA wa operesheni UKUTA wananchi wengi tumegundua mambo mengi sana kuanzia Serikali,Sekta za Umma,Taasisi na vyombo vyote vya Dola ambavyo hatukutegemea kama navyo viko kisiasa.
Hata akiingia kiongozi gani yeyote yule wa chama chochote kile kwa upande wangu ninasema ni Zero kama HAKUNA Katiba mpya.
Haiwezekani Wateule wa Rais wakafanya au kutenda Jambo tofauti na Mteuzi wao anavyotaka,wengi tumewaona wanavyo vunja Katiba na Sheria za nchi.
Hatuwezi fika popote pale pasipo Katiba Mpya isiyo mlinda yeyote yule atakaye vunja sheria ilimradi yuko chini ya jua hili.
Mfano Tumeona Rais wa Brazili yuko nje ya Ikulu sasa kwa kufuja mali za nchi,tunataka kila mmoja awajibike kwa nafasi yake na siyo wako walio juu ya Katiba nchi hii ni ya maajabu kwelikweli yaliyo nje sayari ya Tatu.
Mfano.Mamlaka ya Rais yanatakiwa yapunguzwe kwani yamepitiliza na kadha wa kadha.
Acha niishie hapa tu maana kuna wakati ninapata hasira kweli hasa ninapoona,kusikia na kutafakari Nchi yangu ya kusadikika mambo yanyoendelea na kutokea.
 
Bunge likiwa halina meno/butu kama hili sasa ni kazi bure.
 
tatizo ni katiba hizi kazi ziwe wanaomba na wanafanya usahili live wale watakao shinda vigezo wanapewa kipindi mubashara wanaeleza wanawezaje iyo kaxi wataifanyeje na wamamikakati gani television ya taifa inaonyesha kipindi maalumu watu wanaona mbona wenzetu kenya wanaweza na wanafanya ilo kuanzia majaji mpaka viongozi wa vyama vya michezo wanapewa nafasi za kujieleza na inakuwa huru na haki sio mambo ya kubebana kwa misingi ya ukabila uchama udini undugu na urafiki ambao hauna tija kwa taifa ndo mana utakuta huyu kamteua huyu na huyu kamwondoa huyu au unateua leo keshokutwa unatengua
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom