Viongozi duniani wenye kashfa ya rushwa

Viongozi duniani wenye kashfa ya rushwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
global_map.jpg
EnvGlobalVillage.jpg

Ulimwegu wa leo ni wa utandawazi, hasa kutokana na teknolojia ya internet. Kuna marais mbalimbali duniani wapokea hongo ili kupisha mafanikio katika nchi zao au kujinufaisha binafsi. Je, marais wapi ambao mpaka sasa wako madarakani wanaongoza kwa kupokea rushwa?

images


An influential newspaper in Spain has published what it said were handwritten documents detailing 19 years of secret payments to leaders of the prime minister's Popular Party.
Mariano Rajoy, left, allegedly took €25,200 every year 1997 from a property developer.

images


(CNN)
-- South Korean president Lee Myung-bak apologized to his country for what he called "shameful incidents" involving his family and inner circle on Tuesday.

Earlier this month, his older brother, Lee Sang-deuk was arrested on bribery charges involving two troubled Korean banks. This week, prosecutors in Korea sought arrest warrants for two former aides to Lee on the suspicion of receiving bribes from the same two banks, according to Yonhap, a South Korean news agency.

images

A corruption scandal has overshadowed British Prime Minister David Cameron’s second visit to India, where he was optimistic of clinching lucrative business agreements to ramp up his country’s fledgling economy.

images


Kauli nzito aliyoiandika Absalom Kibanda kuhusu Rais Kikwete
TAARIFA mbaya zinazomhusisha Rais Jakaya Kikwete na tope la rushwa na ufisadi zimesambazwa katika mitandao ya intaneti tangu mtandao wenye utata mkubwa wa Wikileaks ulipochapisha ‘cables’ mpya zinazoihusu Serikali ya Tanzania. Niliseme hili mapema kabisa kwamba, watu tunaoitakia mema nchi hii na tunaoiheshimu taasisi takatifu ya urais ambayo kwa sasa inashikiliwa na Rais Jakaya Kikwete tulifadhaishwa na taarifa hizo za Wikileaks.

Hauhitaji kuwa shabiki wa Rais Kikwete ili ufadhaishwe na taarifa ambazo zinamtuhumu moja kwa moja kiongozi wako mkuu wa taifa na masuala ya hovyo ambayo kama yataachwa kama yalivyo na hata kufika hatua ya kuaminika, yanaweza kuendelea kuiporomosha hadhi ya urais wa nchi na pengine taifa zima. Hivi nani hajui kwamba ni aibu ya taifa na si ya mtu mmoja peke yake, kuwa na kiongozi ambaye thamani yake ni zawadi ya suti tano alizopewa na mwekezaji mmoja. Haya ni matusi. Hii ni fedheha.

Ni kutokana na ukweli huo basi, ndiyo maana sikushangazwa hata kidogo na hatua ya maofisa wanaoshughulikia masuala yanayohusu mawasiliano katika Ofisi ya Rais (Ikulu) wakiongozwa na Mkurugenzi wao, Salvatory Rweyemamu, walipopata wakati mgumu kujibu tuhuma nzito zilizoelekezwa kwa rais.

Maofisa wa Ikulu wangekuwa watu wa hovyo kabisa, iwapo wangeamua kwa makusudi au kwa bahati mbaya kuzipuuza au kujifanya hawazijali, taarifa za kumchafua rais ambazo zilianza kusambaa kwa kasi kubwa kupitia katika kurasa mbalimbali zilizo katika mitandao ya intaneti na ambazo aghalabu zingedakwa au zilishaanza kunaswa na vyombo vingine vya habari nchini. Utakuwa ni mtu mpuuzi tu unayeweza kuyadharau au kuyapuuza maneno au maoni ya mwanadiplomasia wa hadhi ya Michael Ritzer aliyekuwa balozi wa Marekani hapa nchini anayeaminika kuwa chanzo cha taarifa hizo ambazo kwa mujibu wa Ikulu zilikuwa zikilenga kumpaka matope Rais Kikwete.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, Ikulu iliyojitokeza kumtetea kama si kumsafisha Rais Kikwete dhidi ya tuhuma za kupata kupokea hongo ya kusafirishwa kwenda Ulaya na kununuliwa zawadi ya suti tano wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, inafanya hivyo wakati huu hadhi yake katika jamii ikiwa ni yenye kutia shaka. Sina sababu ya kuanza kueleza au kufafanua hicho ninachokiita hadhi inayotia shaka ya Ikulu zaidi tu ya kusema kwamba unahitaji kuwa na akili za mwendawazimu kutamka kwa kujiamini leo hii kwamba Ikulu ya zama za Kikwete inazo sifa za kuitwa; ‘mahali patakatifu’.

Ukiliacha hilo la hadhi ya Ikulu, utetezi na ufafanuzi uliotolewa na Salva na wasaidizi wake kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa rais na ambazo zimeshaanza kuonekana machoni mwa baadhi ya watu kuwa ni za kipuuzi, kwa mara nyingine umethibitisha kwa mara nyingine tena kiwango cha ubinafsi uliovuka mipaka cha ofisi ya rais.
Salva na timu yake kwa sauti za kukaripia wameziita tuhuma zinazoelekezwa kwa rais kuwa ni upuuzi usiopaswa kuaminika na uzushi wenye lengo la kumpaka matope Rais Kikwete.

Utetezi uliofanywa na Salva kwa Kikwete juzi, unafanana na ule uliopata kutolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kwa nyakati mbili tofauti wakati alipojitokeza kwa nguvu kubwa kumtetea rais zama jina lake lilipohusishwa katika sakata la Richmond na Dowans. Wakati Salva akikanusha tuhuma zinazoelekezwa kwa Kikwete na kusema hazina ukweli na zimejaa uongo na viashiria vinavyolenga kuchafua jina zuri na heshima ya Mheshimiwa Rais, anaonekana kusahau au kuweka kando falsafa ya tuhuma kuwa kipimo tosha cha uwajibikaji anayoiamini kiongozi anayemtetea.

Sitaki kuamini hata kidogo kwamba Ikulu inamtetea kiongozi ambaye kwa kauli na matendo yake ndani ya vikao vya serikali anayoiongoza na hata katika chama ambacho yeye ni mwenyekiti wake amethibitisha kwamba ni mtu anayeamini kwa dhati kabisa kwamba tuhuma peke yake zinatosha kumfanya kiongozi aondoke madarakani.
Hivi Salva na wasaidizi wake hawajui kwamba dhana nzima ya kujivua gamba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoasisiwa na kuabudiwa na Kikwete binafsi na kisha akaisimamia kwa matendo ndani ya vikao, mzizi wake uko katika kuziheshimu tuhuma ambazo hata hazijathibitishwa na mahakama? Iweje leo Salva afikie hatua ya kuitisha kikao cha waandishi wa habari na kumtaka yeyote aliye na ushahidi wa tuhuma dhidi ya rais kwamba alipata wakati wowote kupokea zawadi au hongo akauwasilishe ushahidi alionao badala ya kumshauri mtuhumiwa mwenyewe kupima na kuwajibika?

Hivi huyu anayetuhumiwa leo kupitia Wikileaks si Kikwete huyo huyo ambaye ndani ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ameonesha ujasiri wa kufanya kile alichopata kufanya mfalme Kaisari aliyemuacha mkewe kwa tuhuma tu za uasherati hata baada ya uchunguzi kufanywa na kuthibitika kwamba hakuwa na hatia?

Hivi huyu Kikwete ambaye tunaambiwa anatuhumiwa leo kupokea hongo au rushwa kutoka kwa mmiliki wa Hoteli ya Kempinski Kilimanjaro haoni kwamba anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwaonyesha njia wanasiasa wenzake wa ndani ya CCM ambao hata baada ya kutuhumiwa bado wanaendelea kukataa kuondoka ndani ya chama hicho? Ni kwa nini basi anashindwa kuwa mfano kwa kuwaonesha wana CCM wenzake namna kiongozi mwenye tuhuma nzito anavyopaswa kufanya?

Hivi tuhuma anazokabiliana nazo kupitia Wikileaks hazifanani na zile ambazo miezi michache tu iliyopita zilisababisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) akajiuzulu? Ni kwa nini mwasisi wa dhana ya kujivua gamba analikataa gamba ambalo kwa bahati mbaya limemnasa mwenyewe? Ni wazi kwamba jeuri ya kina Salva kumtetea Kikwete imejengwa katika msingi mkubwa mmoja. Woga wa wanachama wa CCM ambao wameufanya kuwa utamaduni wa muda mrefu wa kuwaheshimu viongozi wao wakuu hata katika mambo ambayo wanajua kabisa kwamba, viongozi hao wamefanya makosa ya wazi.

Hivi nani hajui kwamba hata kabla ya tuhuma hizi za Wikileaks ambazo marafiki za Kikwete kama kina Abdulrahman wanamtetea, jina la kiongozi wao kipenzi limepata kutajwa pia, tena mara nyingi tu katika kashfa nyingi nyingine za ufisadi?
Je, wanadhani tumesahau kuwa kama wanavyofanya leo kina Salva hao hao walipata kufanya hivyo hivyo wakati alipotajwa katika sakata la ufisadi wa IPTL miaka ya 1990?
Au wanadhani sote tumepoteza kumbukumbu na hatujui kwamba hata katika kashfa ya EPA kupitia Kampuni ya Kagoda inayoaminika kuiba fedha na kuingiza katika kampeni za urais wa CCM wa mwaka 2005 jina la kiongozi wanayemtetea leo haliwezi kuachwa katika mazingira ya haki na kweli?
Je, kuna Mtanzania anayefuatilia masuala ya kisiasa na ambaye amefanya utafiti wake wa kina ambaye hajui kwamba kwa akili za kawaida kabisa, huwezi ukalitenganisha jina la Kikwete (tena moja kwa moja) katika sakata zima la Richmond na Dowans lililomlazimisha aliyekuwa Waziri Mkuu na rafiki yake mkubwa kisiasa, Edward Lowassa na mawaziri wengine wawili kujiuzulu?
Hivi wakati Salva na wasaidizi wake wanapojitokeza leo na kumtetea kwa nguvu kubwa Kikwete katika sakata jipya la Wikileaks wanadhani tumeyasahau maneno aliyopata kuyasema aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata hilo la Richmond na Dowans, Dk. Harrison Mwakyembe?

Nitawakumbusha.
Alisema iwapo Kamati Teule ya Bunge aliyoiongoza ingeamua kuyaweka hadharani mambo yote waliyobaini wakati wa uchunguzi wao basi serikali nzima ingeanguka! Ikumbukwe kwamba Mwakyembe aliyasema maneno haya wakati tayari waziri mkuu ameshajiuzulu kwa hiyo ni wazi kwamba, kauli yake hiyo ilikuwa ikielekezwa kwa mtu mmoja tu; Rais Kikwete.
Ni kwa nini hakuanguka?
Kwa nini haanguki leo?

Iwapo Mwakyembe alikuwa ana maana tofauti na hiyo, ajitokeze leo hii na kuwaambia Watanzania, alikuwa akimaanisha nini wakati alipotoa matamshi hayo ambayo kwa sababu ya kubebwa na upepo wa ushabiki na unazi wa kisiasa wa makundi ndani ya CCM kauli yake haikupata kupewa uzito hata na wabunge mahiri wa kambi ya upinzani bungeni zama za Bunge la Tisa.

Waswahili wana msemo wao maarufu; mwosha huoshwa. Leo ni zamu ya Kikwete ambaye hata baada ya jina lake kutajwa kwa tuhuma tu katika IPTL, kisha EPA (Kagoda), Richmond na sasa Wikileaks anaendelea kusafishwa na kutetewa eti kwa kuwa tu yeye ni mkuu wa nchi.

Kikwete na wasaidizi wake wanapaswa kujifunza kutoka kwa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye alilazimika kujitoa mhanga na kumtetea kwa ujasiri mkubwa waziri mkuu wake, Frederick Sumaye, aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kupikwa za ufisadi. Utetezi huo alioufanya Mkapa kwa msaidizi wake mkuu, ulivunja nguvu ya genge ambalo sijapata kuliunga mkono hata mara moja la mtandao ambalo hakuna shaka ndilo lililokuwa nyuma ya tuhuma dhidi ya Sumaye na wanasiasa wengine zama za Serikali ya Awamu ya Tatu.

Kikwete kwa kauli na matendo halitaki hilo. Anajiona yeye peke yake. Anaamini katika dhana iliyopata kumponza mzee Cleopa Msuya isemayo; ‘kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.’ Katika misingi ya uongozi inayoamini katika uwajibikaji wa pamoja hili haliwezekani. Kikwete na kina Salva wanajidanganya. Ni wazi kwamba Kikwete amethibitisha pasipo shaka kwamba, amekuwa ni mtu wa ‘kushangilia’ kila mara wanaposhambuliwa wanasiasa wenzake ndani na nje ya CCM.

Akiwa Mkuu wa nchi, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama na Mwenyekiti wa taifa wa CCM, Kikwete amekuwa kimya na wakati mwingine akifanya masihara ya wazi wakati viongozi wenzake wanaposulubiwa hata katika makosa ambayo ama waliyafanya kwa pamoja au wanazushiwa kwa sababu tu za kisiasa. Tabia yake ya kuwaacha viongozi wenzake wasulubiwe na kuwatwisha mzigo wa kujitetea wao wenyewe hata katika mambo ambayo serikali inawajibika moja kwa moja, ndiyo iliyosababisha kwa zaidi ya miaka sita sasa serikali ikwame na ielemewe na tuhuma ambazo baadhi yake hazina mashiko. Matokeo ya tabia yake ya kutaka yeye peke yake ndiye aonekane akiwa safi na salama ndiyo ambayo imewafanya maadui na marafiki zake wamwite kila aina ya jina baya.

Wako waliomwita msaliti, wengine wakampachika jina la msanii na wengine kwa sababu ya kukatishwa tamaa na aina yake hii ya uongozi usiojali mambo au unaopuuzia masuala ya msingi, wakamuona kuwa ni kiongozi ‘mswahili’. Sifa hizi hastahili kuwa nazo kiongozi mwenye dhamana kubwa na nzito kama alivyo. Yeye na timu ya wasaidizi wake ikulu, serikalini na ndani ya chama anachokiongoza wanapaswa kutambua kwamba ni jambo lisilowezekana kuwaita kila wanaomtuhumu yeye kuwa ni wazushi isipokuwa tu pale wanapotuhumiwa viongozi wengine. Hana sababu hata moja ya kusubiri kujifunza kwa viboko.


Makala hii ilichapishwa mara ya kwanza Septemba 7, 2011 katika safu yake ya Tuendako alipokuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti hili.

Tanzania daima 25, March 2013


 
Lakini kwenye ile "List of Shame" ya Dr Slaa, Dhaifu yuko namba 11 na hajawahikanusha!!
 
Lakini kwenye ile "List of Shame" ya Dr Slaa, Dhaifu yuko namba 11 na hajawahikanusha!!
Hongo la suti tano
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, Ikulu iliyojitokeza kumtetea kama si kumsafisha Rais Kikwete dhidi ya tuhuma za kupata kupokea hongo ya kusafirishwa kwenda Ulaya na kununuliwa zawadi ya suti tano wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, inafanya hivyo wakati huu hadhi yake katika jamii ikiwa ni yenye kutia shaka. Sina sababu ya kuanza kueleza au kufafanua hicho ninachokiita hadhi inayotia shaka ya Ikulu zaidi tu ya kusema kwamba unahitaji kuwa na akili za mwendawazimu kutamka kwa kujiamini leo hii kwamba Ikulu ya zama za Kikwete inazo sifa za kuitwa; ‘mahali patakatifu'.

Hili hongo la suti tano walionaje? Je, ni kisa cha kuteswa Kibanda?
 
images


A Nigerian legislator who led a probe into the nation's fuel subsidy programme that saw billions of dollars lost through fraud has been charged with allegedly soliciting a $3m bribe from someone targeted by the inquiry
 
_60050493_kikwetecabinet.jpg

Tanzania's President Jakaya Kikwete has sacked six ministers amid allegations of government corruption.
He has been under pressure to deal with the scandal following a report by a body overseeing public finances. The inspector of the government's accounts noted the rampant misuse of funds in at least seven ministries.
The ministers who have been dropped from cabinet all hold high-profile portfolios: Finance, energy, tourism, trade, transport and health.

BBC
 
[h=2]
images

Fifa president Sepp Blatter has admitted the 'cash for votes' World Cup 2018 bribery scandal has had a "very negative impact" on the world governing body.[/h]
 
images

At its peak in the 1990s, Lai Changxing's smuggling empire transported chemicals, cooking oil, tobacco and cars. He had hundreds of police, customs officers and government officials on his payroll in the southern port city of Xiamen, which he ran like his own personal fiefdom. But the law finally caught up with Lai: he was sentenced yesterday to life in prison for smuggling and bribery in a corruption case that reached into the highest echelons of the Communist Party and involved a 12-year extradition battle with Canada. "The crimes involve massive sums and particularly serious circumstances," court officials told the Xinhua news agency.
 
former-pm-lowassa-340_227.jpg

Tanzania's failure to enforce anti-corruption laws in light of a recent energy scandal is a sign of a politicised justice system, analysts say.
Minister for Energy and Minerals Sospeter Muhongo, supported by a number of parliamentarians, accused the Parliamentary Standing Committee on Energy and Minerals of accepting bribes from companies vying for energy tenders.In response, on July 28th, National Assembly Speaker Anne Makinda disbanded the 28-member energy committee on corruption allegations.
 
images

The slaughter of elephants and the seizure of illegal ivory have soared to their highest levels in decades. A voracious market in Asia and chaotic wildlife protection in much of Africa have put elephant herds at risk throughout the African continent, particularly in Central and East Africa. Poachers are gunning down whole families, oblivious to game scouts.
A key battleground is Tanzania, one of the world's last great repositories of elephants. Perhaps 70,000 to 80,000 elephants roam this nation's immense sanctuaries, amounting to perhaps a quarter of all African elephants. In colonial times, the Tanzanian island of Zanzibar held the largest ivory auctions in the world. Today Tanzania has regained that infamy. Those public auctions have been replaced by underground networks of smugglers, but Tanzania remains a leading source of ivory. From 2009 to 2011, the country was the leading exporter of illegal ivory in the world. Thirty-seven percent of all elephant tusks seized by law enforcement came from Tanzania, with neighboring Kenya a close second.
 
images

Tanzanian Affairs has been giving prominence in recent issues to reports on the various corruption cases which have been widely and frequently debated in Parliament, the media and elsewhere.


Kikwete – "578 Cases in court"

In a historic first ‘question and answer session' broadcast live on all major television and radio networks on September 9, President Kikwete answered many questions, from around the country, on corruption. "We have taken steps and, as we speak, there are 578 corruption cases in the courts" he said. He added that the number was only 58 in 2005 when he had assumed power. He brushed off claims that his government was harbouring people suspected of grand corruption within the government and the ruling CCM party.


He also dismissed claims that the ruling party of which he was Chairman, was silencing MP's who spoke out about corruption in the National Assembly. He also cited cases currently going on in various courts as well as senior public officials who were facing charges of abuse of office and embezzlement. He said that the respective anti-corruption agencies were finalising two or three cases involving high-profile personalities. "Our party would like MPs to speak out and assess their government" he said, "but that should be done in a way that protects the party's interests too."


Tanzania drops 24 places

A few days later, the international Berlin-based anti-corruption watchdog ‘Transparency International (TI)' released a report showing that Tanzania had dropped 24 places in the ‘Global Corruption Perception Index (CPI)' from the 102nd position in 2008 to the 126th spot in 2009.
The CUF Leader in Parliament, Hamad Rashid Mohammed, said the Judiciary did not act fast to clear pending corruption cases, while the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) was dragging its feet in investigating allegations of grand corruption. Hamad told The Citizen that, although Parliament had been at the forefront in the fight against graft, many corruption scandals had been exposed but the Executive and Judiciary had so far done nothing.
Another government critic said that many corruption suspects were being acquitted because of the PCCB's ‘shoddy investigations' and its failure to effectively prosecute those charged with corruption.
The PCCB Public Relations Officer said she had not seen the TI report, but added that reports that Tanzania had fared better than other East African countries were ‘encouraging'. Rwanda had won accolades for wide-ranging steps to improve governance and gone up 14 positions to break into the top 100. Burundi, the worst performer in the region, was ranked 168th. Tanzania's best ranking was 94 in 2007, when Parliament finally set up the PCCB.

The long-running Richmond saga (see earlier issues of TA)

The investigative newspaper ‘This Day' revealed in October that, in addition to all the other irregularities, the controversial Richmond Development Company (which had later become Dowans Holdings), had tried to obtain more than $115 million from the government in 2006 for capacity and energy charges, under the later badly discredited emergency power supply contract it had signed. But, according to the paper, this represented a hefty profit as it had only spent $30m to install the planned 100-megawatt power plant in Dar es Salaam.


According to government sources quoted by the paper, Richmond/Dowans was subsequently paid more than $42m. The government had also paid $4,865 (approx. Shs 6bn/-) for airlifting some of the power generators, consumables, and other accessories from the United States. But, apparently, what the company brought in was only 20MW of power generating sets – one fifth of what was needed under the contract. This however, still represented a hefty profit for Richmond, considering that the company spent just $30 million to install the plant in Dar es Salaam.
Dowans Holdings apparently bought the remaining power generators from South Africa. But a government technical team sent to Cape Town in December 2006 to assess the trailer-mounted turbines, was said to have discovered that some of the equipment was rusty.

The formal termination of the contract between Richmond/Dowans and the government in 2009 paved the way for certain persons to set in motion yet another plan to obtain $69 million by selling the power generators to the government. It was only the fierce opposition to the proposal mounted by the parliamentary Energy and Minerals Committee and others, that blocked this from going ahead.
Towards the end of last year, while some MP's were becoming increasingly restive as they waited to hear the government's reactions to the numerous recommendations in the parliamentary report dated February 2007, the government announced that it intended to resurrect the company, as electricity supplies were again proving inadequate – The Guardian. In October 2009, according to the Guardian, there was some surprise, amid escalating power rationing, that the government's call for tenders for new emergency power generating plants failed to attract any competent bidders.

Government takes over and starts producing electricity

Eventually President Kikwete directed the appropriate ministers to take over the plant, which had been idle for several years, from its liquidators, to ease the crippling shortage of electricity.
Standard Chartered Bank (Hong Kong) then told the High Court that this decision was contrary to a court order that had placed the company under receivership and asked the court to halt the move as it would be unfair. The case was adjourned – Mwananchi. During November the plant finally began producing electricity.
 
photowide

The Judiciary of Tanzania, the country's highest legal authority, is the latest institution to fall under the shadow of corruption following the arrest and prosecution of primary court magistrates who are accused of receiving bribes. Several magistrates in lower courts have appeared before the court over the last five years to answer charges of receiving bribes with intent to influence court decisions. These charges paint a potentially disturbing picture of the country's judiciary.
 



Hivi huyu anayetuhumiwa leo kupitia Wikileaks si Kikwete huyo huyo ambaye ndani ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ameonesha ujasiri wa kufanya kile alichopata kufanya mfalme Kaisari aliyemuacha mkewe kwa tuhuma tu za uasherati hata baada ya uchunguzi kufanywa na kuthibitika kwamba hakuwa na hatia?

Hivi huyu Kikwete ambaye tunaambiwa anatuhumiwa leo kupokea hongo au rushwa kutoka kwa mmiliki wa Hoteli ya Kempinski Kilimanjaro haoni kwamba anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwaonyesha njia wanasiasa wenzake wa ndani ya CCM ambao hata baada ya kutuhumiwa bado wanaendelea kukataa kuondoka ndani ya chama hicho? Ni kwa nini basi anashindwa kuwa mfano kwa kuwaonesha wana CCM wenzake namna kiongozi mwenye tuhuma nzito anavyopaswa kufanya?

My take:

Duh, kweli Kibanda ni mwiba. Kwa mtindo huu, wahusika wa utekaji wake lazima iwe kitendawili.

 
meno na kucha zangu nazithamini kuliko mdomo na keyboard nyumbani na mwambepande we unatamani wapi?
Wanajamvi baba mwanaaasha alisema anataka aenziwe au akumbukwe mema au mabaya hamwoni mnamkosea baba adabu
 
Candid Scope, J. K na serikali yake wanapaswa kutoa majibu juu ya utekaji na uteswaji wa Kibanda.

Kama ni habari hii ndiyo yenyewe imejitosheleza haswa ktk suala zima la rushwa za huyu ------.

Serikali ya ------ tuambieni nani wamemtesa Kibanda? Na hapa tume-foward kwa sababu ya Ulimboka bado mnapiga danadana.

Uwezo mdogo wa kutotaka kufikiri, kuuliza, kuchambua ili upate jibu sahihi ndiyo tatizo la serikali ya ------. Always wanarahisisha mambo, 97-9=7
 
Back
Top Bottom