Kuna uhusiano gani wa viongozi wakuu wa CDM na kuwahi kufanya kazi BOT?
1. Mzee Mtei alipata kuwa Gavana wa BOT
2. Marehemu Bob Makani alipata kuwa Naibu Gavana wa BOT
3. Freeman Mbowe alipata kuwa Ofisa wa BOT
NB: Kunanini BOT na kuja kuwa kiongozi wa CDM?
Hilo la Mtei na Mbowe, ni baba mkwe na mkazia mwana. Kuna nini cha kushangaa hapo? hakuishia kumoa kazi BOT bila kuwa na vigezo, akaja kumrithisha na Uenyekiti wa chadema.
Mtei na Bob Makani wote waliajiriwa na Nyerere.
Isitoshe, ukifatilia uanzishwaji wa vyama vya upinzani Tanzania utajuwa kwanini.
Enzi hizo, wakati mfumo wa vyama vingi unarudishwa tena kwa shinikizo la Mataifa ya nje, hakuna hata chama kimoja cha upinzani wa kweli kilianzishwa na wapinzani wa ukweli kikasajiliwa. Vyama vyote vilianzishwa na watu ambao walikuwa handpicked na UWT.
Anko Zomba huwa anasema wote hao, Mtei, Bob, Mbowe, Sefu, Lipumba, Mbatia, Mrema, Bwana Mapesa "ni system tu". Hakuna jipya.