VING'AMUZI NANI AMLIPE NANI nini?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Walionunua ving'amuzi vya Azam, DStv, Zuku walifahamu kabla ya kuvinunua kuwa ni vya kulipia.
Walivinunua kwa kazi nyingine, sio kwaajili ya kuangalia TBC, ITV, Channel ten, Clouds na Star tv kwakuwa mara nyingi wateja wenye ving'amuzi vya Azam, DStv na Zuku wengi wao wana ving'amuzi vingine pia, hasa vya StarTimes, Digitek au Ting.
Mfano, mimi nina ving'amuzi vya StarTimes, Azam na DStv. Mtu kama mimi siwezi kudai au kuwalaumu Azam na DStv kuwa wameniibia, maana nilijuwa kabla na lengo langu halikuwa kuangalia FTAs kwa kuwa nilikuwa na king'amuzi cha StarTimes ambacho hata hicho ilikuwa lazima ulipe ili kuona FTAs except TBC1.

Hata TBC, ITV, Channel ten, Clouds na Star tv wenyewe walikuwa pia wakijisikia fahari kwa matangazo yao kuonekana DStv ambayo inaonekana mbali na yenye wateja wengi Afrika. Walikuwa wanatoa maelekezo ya namna wateja wao wanavyoweza kuwapata (channel number) kwenye king'amuzi cha DStv.

Hii inaonyesha kwamba FTA ndizo zilizostahili kuwalipa Azam na DStv kwa kuyasafirishia mbali kwenye soko kubwa matangazo yao kinyume na madai ya sasa.

Kwa upande mwingine kama wako wateja ambao walinunua Azam, DStv na Zuku kama sehemu ya kupata maudhui ya ndani kama ilivyokuwa wakati wa analog hawa watakuwa wamejichanganya wenyewe.

Sasa lazima hesabu zipigwe kuona nani alikuwa akifaidika kati ya pay TVs waliokuwa wanasafirisha matangazo ya FTAs hadi Nigeria na SA na FTAs ambazo zinaandaa matangazo ya tv yanaoyoishia kuonekana kwa wateja wa Magomeni na Kibamba tu.
 
Ivi ""TCRA"" wanawachukulia poa DSTV. Serikali imewashindwa ""ACACIA"" itawaweza DSTV.
Hawa watu wanafanya bihashara kwa mikataba na sheria makini, ambazo zipo na zimesainiwa na mahakama kuu za bihashara uko British na USA. Kama wanataka mabepari wanyanyuke na ndege zao kutoka Ulaya na USA waje kueleweshana ktk mikataba haya
 
Hayo mambo mi yananiumiza kichwa tu,wanajifanya serious kwenye habari lakini mambo mengine wanarushiana mipira
 
Back
Top Bottom