Yusomwasha
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 2,092
- 838
Yaani usipolipia ni full uhuni inabaki TBC tu kuanzia Azam,Zuku,DSTV, Continental na TING.
Yaani hakuna afadhali sijui itatupasa tuwe na ving'amuzi lukuki ndani tumewachoka TCRA ni jipu.Hawa TING walikuja na kuangalia bure bila kulipia yaani sasa hivi hawafai tena.
Continental walianza vizuri wakasema ni bure tena ni quality watu wakanunua na channel kibao sasa hivi hawafai kabisa kinaskrach balaa malipo ndo usipime kuna malipo mpaka ya siku kila siku buku, halafu customer care wabovu kama hawa sijapata kuona yaani wana majibu mabaya sana.Ving'amuzi vyao ni ghali balaa tena vibovu ukinunua kwa mtu mwenye kipato cha chini utapata shida.
Hawa zuku nao hawafai dishi lao bei chee ila utajuta si rafiki wa mvua yaani kulipia vifurushi vyake ni ghali halafu wamerundika channel za kikenya tu
Hawa labda wajirekebishe.
DSTV nao inabaki TBC vifurushi vyao viko juu sana lakini wapo vizuri ni full digital ila wanatunyonya sana na gharama zao.kwa mtu wa kipato cha kawaida usinunue hii.Sitawalaumu sana DSTV maana wao ni kimataifa zaidi.
Kuna hawa startimes yaani wana ving'amuzi type nyingi kuna vya zamani venye local channel za bure na kuna hivi vya sasa hivi ambavyo ni balaa tupu inabaki tbc tu tena hawana huruma.Customer care yao ni mbovu sana na vinaskrach sana yaani hawa kama wameingia digital nahisi waliingia bila kujipanga.Bei za ving'amuzi vyao hazieleweki kabisa.
Kuna hawa AZAM yaani hawa walikuwa tegemeo kwa watanzania lakini sasa hawafai tena. Visimbusi vyao ni ghali sana halaf nao kifurushi kikiisha inabaki TBC. Wamepandisha gharama ya vifurushi sana. Yaani azam wangeshusha gharama ya madishi yao na wakiweka vifurushi vya chini kama Startimes wangekua mbali sana lakini wanaboa.
Azam onyesheni EPL hapo mtakua mmeiacha DSTV mbali. Punguzeni gharama ya vifurushi na dikoda zenu.
Mwisho kabisa naomba TCRA mchukue hatua dhidi ya hivi ving'amuzi bila hivyo mjiuzulu kwa kushindwa kazi na mtatumbuliwa