Nakumbusha kuwa msingi imara wa CDM siyo personalities bali mfumo wa utendaji wa chama. CCM wanalijua hilo ndiyo maana ya thread za akina TUNTEMEKE & co.
Tusiruhusu huu mfumo wa utendaji wa chama ukaingiliwa na kirusi cha madaraka kwa kuwabambikia madaraka watu kwa matukio.
Uchaguzi huu pamoja na wa madiwani umethibitisha kuwa
1, Maamuzi ya pamoja yana toa fursa ya kuwajibika pamoja kupitia "defined chain of command"
2 Unatoa fursa ya kujengana na kubadilishana uzoefu
3. Jamii inapata fursa ya kutambua hazina na fursa mbadala wa makamanda wao.
4. Unaibua vipaji na kujiamini kwa individauls wanaopewa fursa ya kutekeleza hayo majukumu.
5. Maadui wanashindwa ku zero kumshambulia mtu binafsi ndani ya mfumo
KINYUME CHA HAYO NDIYO DONDA NDUGU LA CHAMA TWAWALA LA GANZI YA MAENDELEO TANZANIA
nimemkubaliV. Nyerere ni mashine acha kabisa
You are right!Pongezi pia ziende kwa kamanda wa kampeni hizo John Mrema, Vicent amefanya kazi nzuri jukwaani lakini mikakati yote na utekelezaji wake ni John Mrema ambaye hapa alizusishiwa mengi ili kukatishwa tamaa lakini hatimaye kwa kushirikiana na viongozi wenzake wamefanikisha ushindi
Hongera CCM kwa kukubali kushindwa. Mimi ushauri wangu kwa akina Nape na wenzake ni kuwa wawashauri vikongwe wa CCM kuwa sasa muda umefika wa kuwaachia hatamu za uongozi vijana ndani ya chama. Mkakati wa kutumia akina Wassira hautafanikiwa sana kwani kutakuwa na wapiga kura wapya wengi ifikapo mwaka wa 2015 yaani waliozaliwa 1997. Pia huu mtindo wa kutoa fursa kwa kuangalia majina ya viongozi waliopita kwa sasa unawaagusha sana, Najua Nape NNAUYE ni mmoja wa wafaidika wa mfumo huo lakini ukweli ni kuwa unakifanya chama kuonekana kuwa cha kisultani zaidi. Nimesikia hoja zikitolewa na CCM wakati wa kampeni za Arumeru kuwa mbona na CHADEMA nao wanafuata mtindo huohuo na walikuwa wakitoa mfano wa jimbo la Moshi. Ukweli ni kuwa makosa mawili hayawezi kufanya jambo liwe sahihi. Mwisho ni suala zima la ufisadi ndani ya chama na matumizi ya mafisadi kwenye kampeni. Acheni hilo mara moja.
No comment labda tumuulize Mkapa "eti Mr Clean Huyu Kiboko wako tumpe cheo gani ili kila ukimsikia masikio yako yatoe moshi!" lol am kidin!!
Umenifurahisha sana kuhusu kulialia kwa kina Tuntemeke, TII, na PAA sijui wamepotelea wapi.Ni mapema sana kuzungumzia vyeo saizi, ngoja tusherehekee kwanza na kupeana pongezi. Vince was a mastermind na CDM itumie uzoefu wake kwa chaguzi zingine but sidhani kama ndio cheo kitafutwe kwa ajili yake. Vyeo ndio chanzo cha migawanyiko katika vyama. Kuna makamanda kibao wamepigana kuga na kupona Arumeru so watataka nao kupewa ka cheo fulani kama mwenzao Nyerere na wakinyimwa wataanza kulialia kama Tuntemeke, tii na paa