Vinavyotuua Watanzania : Mamlaka husika hazina meno

Vinavyotuua Watanzania : Mamlaka husika hazina meno

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Wakati kuna vyombo vya usimamizi ikiwemo BODI ya Maziwa Tanzania , Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) ambavyo vinahusika kuhakikisha inaratibu kiwango vya ubora wa maziwa hapa nchini ili kulinda afya za walaji, kumekuwa na baadhi ya makampuni ambayo yanazalisha bidhaa hiyo pasipo kuzingatia viwango.

Katika pita pita yangu kwenye baadhi ya maduka, leo nimekutana na mtindi unazozaliwaha ka Kiwanda cha Maziwa cha Mara Msoma. Katika kifungashi (Chupa) kumebandikwa maelezo (Label) yenye Nembo ya TBS ambayo inasoma kuanzia mwaka 2012 mpaka 2017. Wakati inaonekana kuwa mtindi huo umetengenezwa katika batch moja, lakini kuna baadhi ya label zimewekewa vema (tick) kwenye mwaka 2012 na nyingine 2013 Ila cha kushangaza kama mnavyoweza kuona hapa kuna mengine yamewekewa vema kwenye Dec 2017.

Wataalamu wa Maziwa mnaweza kutusaidia, hata kama maziwa yakiwa kwenye chombo cha kuhifadhia (Kopo kama hili) Je, yanaweza kukaa miaka zaidi ya minne pasipo kupoteza ubora wake??

Hii ni hatari sana kwa walaji ikichukuliwa kuwa wapo watanzania ambao hawajui au hawana upeo wa kutambua "expiry dates" kwenye bidhaa. Maziwa haya yapo sokoni na ubora wake unapimwa kwa kuwekwe vema na peni tu kwenye mwaka wowote. Nimejaribu kufungua hiyo chupa kwa kwenye mtindi huo unatoa harufu kama pombe na umeumuka utadhani umewekewa amila muda huo huo ....

Watanzania tunakwenda wapi?? watu wanafikiria faida kuliko maisha ya wenzao...Mamlaka husika hazitekelezi kikamilifu majumu yake kikamilifu, hazipiti madukani kukagua na kuondoa bidhaa feki ili zisihashiri afya za walaji. Watengenezaji wa biahdd nao wapo kimya, hawafuatili kujua bidhaa zao zinaangaliwa vipi kwenye maduka ya reja reja..

Katika nchi zilizoendelea, ni kosa chini ya Sheria za Ushindani wa Haki (Fair Competition legislation ) na zile za kulinda walaji (Consumers Protection Laws) au za viwango (Products Control Regulations) kwa mtengenezaji wa bidhaa , sambazaji au muuzaji wa reja reja ambae anaacha bidhaa iliyopitwa muda wake kwenye "shelves" za duka au stoo.

Vyakula ndio chanzo kikubwa cha matatizo ya afya zetu. leo tunalishwa vyakula vilivypitwa muda wake, tunalishwa unga uliotokana na mahindi yaliyopulizwa DDT na sumu nyingine kali, tunakula mchicha na matembele toka mto Msimbazi na kweningne ambapo maji yanayotumika yana kemikali hatarishi.

Mamlaka husika zipo tu na hazichukui hatua staili. Tunapopigiwa kampeni ya kunawa mikono, kuchemsha maji, kutumia vyandarua, kutofanya mapenzi bila kondom nk nk...mahali pengine tumesahau kuweka mkazo hivyo tunajikuta tukipoteza maisha taratibu...


 

Attachments

  • Mara 1.jpg
    Mara 1.jpg
    35 KB · Views: 41
  • MARA exp.jpg
    MARA exp.jpg
    37.5 KB · Views: 43
  • mara youghut1.jpg
    mara youghut1.jpg
    48 KB · Views: 45
  • mara2.jpg
    mara2.jpg
    12.3 KB · Views: 47
Back
Top Bottom