Hii inanikumbusha utetezi wa lowasa aliweka mkataba wa kinyonyaji wa Richmond kwa maelekezo ya kimemo cha mdomo.
Watu kulalamika hata kisicho na kweli,
Yeye kama rais alisema waliokwepa kido waende wakalipe,majina ya watumishi waliotumia nafasi zao kusaidia watawajibishwa
So suala la vimemo aliyeandika kimemo na alikipokea watajuana sisi tunataka kodi zetu
Kama ni hivyo basi juhudi hizi anazofanya na kusifiwa Mhe Magufuli zinaweza kuishia na fedheha kwake. Maana huwezi kuwa unasema unadhamira ya kupambana na ufisadi na rushwa halafu baadhi ya wahusika ukawaficha ili kuwalindia heshima huku wengine ukiwasulubu.
Tunataka MAJINA ya wote waliohusika na kuwa amuru maafisa wa TRA na Bandari kwa vimemo watende maovu.
mzeelapa toka lini adhabu ya mlipa kodi ikawa ni kulipa ushuru?
Kisheria mtu aliyekwepa kodi anatakiwa kukamatwa, kushtakiwa na kufilisiwa mali ili kulipa fidia ya kodi aliyoikwepa Nukta.
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.
Tufanye kwa mfano Rais au PM alimwandikia Kamishna wa kodi aondoe kontena fulani bila kulitoza jee huoni hiyo ilikuwa ni amri hata kama ilikiuka sheria? Na kama unamwajibisha huyo Kamishna wa kodi kwa kosa hilo jee hutakuwa umemwonea kama utakuwa hujamwajibisha na yule aliyetoa amri?
spot on, watanzania tusiwe washabiki wa vitu visivyo na tija, sisi tunachotaka waliokwepa kodi washajulikana na sheria inasema tuwabane watulipe kodi yetu basi aliyeandika memo na muandikiwa watatafutana wenyewe uko mitaana warudishiane pesa walizopeana ili kodi yetu ilipwe tuache kushabikia vitu visicvyo na tija wala haviongez pato la tafia rais ana mambo mengi ya ku deal nayo kuliko haya tu
It is true.Hapo ndio kwenye mwamba, drill bits zinaumana na jiwe. Utasikia ukimya baadaye tutasahau.
Sakata la makontena bandarini limeonyesha jinsi nchi ilivyokuwa imeoza na kuwa inapoteza fedha nyingi za umma huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendesha huduma za jamii.
Kuna watu wazito wamepoteza kazi na wengine bado wanashighulikiwa na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Lakini habari zilizopo ni kuwa mengi ya makontena hayo yalikuwa yanatolewa kwa vimemo kutoka kwa wakubwa serikalini kwa maana hiyo hao wameshiriki kuhujumu nchi kwa madaraka yao na kusababisha madhara tunayoyaona ya kukosekana kwa huduma nyingi ikiwemo madawa hospitalini iliyopelekea Watanzania wengi kufariki dunia.
Je, ni nani hao waliokuwa wanaandika hivyo vimemo? Waziri mkuu kesha pewa baadhi ya vimemo hivyo, je sasa hivi si ndio wakati muafaka wa kuweka hadharani majina ya wahusika bila kujali vyeo vyao ili tuweze kumuamini yeye na bosi wake Rais Magufuli kuwa wanayofanya sio maigizo bali ni dhamira ya kweli?
sakata la makontena bandarini limeonyesha jinsi nchi ilivyokuwa imeoza na kuwa inapoteza fedha nyingi za umma huku nchi ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa fedha hivyo kushindwa kuendesha huduma za jamii.
Kuna watu wazito wamepoteza kazi na wengine bado wanashighulikiwa na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Lakini habari zilizopo ni kuwa mengi ya makontena hayo yalikuwa yanatolewa kwa vimemo kutoka kwa wakubwa serikalini kwa maana hiyo hao wameshiriki kuhujumu nchi kwa madaraka yao na kusababisha madhara tunayoyaona ya kukosekana kwa huduma nyingi ikiwemo madawa hospitalini iliyopelekea watanzania wengi kufariki dunia.
Je, ni nani hao waliokuwa wanaandika hivyo vimemo? Waziri mkuu kesha pewa baadhi ya vimemo hivyo, je sasa hivi si ndio wakati muafaka wa kuweka hadharani majina ya wahusika bila kujali vyeo vyao ili tuweze kumuamini yeye na bosi wake rais magufuli kuwa wanayofanya sio maigizo bali ni dhamira ya kweli?
Ingekuwa vizuri vikakusanywa ili kuwabaini walioviandika na kutambua vilisababisha madhara kiasi gani kwenye ukusanyaji kodi kisha wabanwe ipasavyo na sheria ichukue mkondo wake.
Hilo ndo la maana tukianza vimemo na vikachunguzwe kodi zetu hawatalipa au watatuchelewesha,ili siku NYINGINE ambao bado wako kwenye mtumishi hawatakubari kuingizwa mkenge wa vimemo,vinginevyo vinaandikwa na wake /mahawala wa viongozi wanagonga muhuri ndo vitupoteze muda,
Wahusika wanatakiwa kulipa ushuru wa makonteina yao nukta. Mambo ya vimemo, kama walivinunua au kutoa rushwa watajuana wenyewe kwani mtu hawezi kupindisha taratibu na sheria kwa vimemo.
Very good! Sisi tuhangaike na yule aliyeruhusu. Mambo ya nani alitoa kijimemo sisi hayatuhusu. Huyo aliyepokea kimemo na kukifanyia kazi wakati akifahamu anavunja sheria, hiyo ndo balaa kwake.