Mhhhh! ni uwongo uliomithilishwa na ukweli huku CCM hakuna mwenye akili hiyo (strategic planning) hata Idara zetu za hamasa hazina, kinachofanyika ni "to capitalise on events" hili la Lipumba sasa nakuhakikishia Lumumba hakuna anayelijua kama mkono ni wa serikali na baadhi ya wanaCCM nje ya Lumumba ingekuwa hili linajulikana Lumumba ungeona a co-ordination response, sisi kwa sasa tunatafuta ni namna gani ya ku "capitalise" na mgogoro huu lakini ngumu na hasa kwa maneno yaliokuwepo kwamba CCM ina mkono tuzaweza tukawacha "foot print" mbaya kwa hiyo tunaangalia tu linavyokwenda na litakavyoisha, kama ndani ya CCM yuko anaelijua basi itakuwa Mkware na idara maalum zake zake tu na some few brains kama Dr. Ramadhan Dau na wale waliokuwa karibu na Lipumba Mtaa wa Idrisa..
Mtumbatu,
Unaandika vizuri na sina shaka yoyote kuwa hapa nazungumza na mtaalam.
Ukitaka kuliona hili vizuri inahitaji urejee nyuma sana katika historia na uangalie
vipi ''watu,'' hushughulika na mikasa kama hii.
Umesema kweli kuwa kunakuwa na hofu ya kuacha alama za miguu na njia ya
kulikwepa hilo ni kukaa pembeni ''watu,'' wakaachiwa wachezeshe mchezo.
Alama za miguu zinaonekana kupitia wachezeshaji.
Ukisoma gazeti la Uhuru utapata ujumbe ulio wazi kabisa na kwa aliyepitia haya
hashindwi kufahamu kuwa ni punda milia yule yule ila kabadilisha miraba tu.
Mimi binafsi nimejifunza katika kile kilichokuja kujulikana kama, ''mgogoro wa
East African Muslim Welfare Society.''
Closer to home, Kambi ya Kipumbwi, Tanga katika Mapinduzi ya Zanzibar, 1964.''
Wapo lakini huwaoni sharti na wewe uwe mwanga kama wao.