Uchaguzi 2020 VImbwanga tarajiwa katika uchaguzi mkuu 2020

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
237
500
VIMBWANGA TARAJIWA
Jinsi tunavyoukaribia uchaguzi mkuu ndivyo tutakavyo shuhudia vimbwanga. Jiandaeni kwa muvi zifuatazo:

1. Ugomvi wa kugombea bendera mtaa wa Ufipa. Zitapigwa kavu kavu baina ya aliyenunua Chama na aliyeigiza sinema ya HE GOES TO NAIROBI. Mshindi piga ua atakuwa mnunuaji Chama. Ugomvi huu utazua kuhujumiana kwenye kampeni na utafuatiwa na Ile wimbo maarufu wa kwaya ya Hai unaojulikana kama TUMEIBIWAAA na ubeti wake wa HATAAPISHWAAA.
...
2. Ugomvi ndani ya MAWESE PARTY ugomvi ambao kiini chake haswa utakuwa ukosefu WA hela. MAWESE PARTY itashindwa kuwawezesha wagombea na hapo ndio KING MAWESE atapata tabu saana kutoka Kwa wenzake. Ugomvi huu unaweza kuisha Kwa KING MAWESE kuhamia mtaa wa Ufipa na kuwaacha kina Mawese chipukizi kwenye mataa. ILA nao watadai alikuwa TAKATAKA aende zake. Hapo ndipo Mzee WA TAKATAKA Katibu MWENEZI atapanda cheo.

3. Kuna Mzee mmoja toka kulee ng'ambo ambaye bado anaota ni kiongozi wa KAFA. Atakuja kutahamaki siku ya kuchukua form ofc za time atakapoambiwa hatukutambui. Huyu naye fasta atapiga breki mtaa wa Ufipa kutafuta hifadhi.

4. Kutakuwa na kile kikundi cha matarumbeta kikiongozwa na Mzee WA kuhamisha Bahari Dodoma. Hawa watacheza kote na popote mradi mshiko uwepo. Wanaweza kurubuniwa kuungana lakini wajanjaa watahepa. Swali utakuwa waachiwe majimbo gani? Maana hawana Jimbo hata nusu! Kwenye muungano ni liability than profit! Kama kawa hawataacha kuingia na kutoka mtaa mkubwa wa Lumumba. Walau watoto waende Choo.

5. Kampeni zifuatazo kutakuwa na gharika aka Tsunami. Itakuja na mjenga SGR, mnunua ndege! I
Ule upande wa mafuriko utakuwa na ukame na kipindi kigumu cha joto huku upepo ukivuma kutoka baharini kuelekea Chato.

6. Majimbo ya kina Sugu, Lema, Lissu, Halima, Mnyika, Kubenea, Msigwa, Mbowe, Zitto yatashuhudia mtafaruku mkubwa mno ambao utapeleka kilio cha mbwa mwizi mtaa wa Ufipa.

7. DP itazuiwa kushiriki uchaguzi mkuu kutokana na wao wenyewe kuwekeana mapingamizi.

8. NLD na NCCR zitaendeleza mkakati wao wa kujibanza mvua upenuni mwa nyumba ya jirani. Na Kwa kufanya hivyo vitakuwa vimefikia mwisho wa uhai.

9. TLP ndio Chama pekee kitakachokubali matokeo na kitashiriki sherehe ya kumkabidhi mshindi cheti kikichukuwa nafasi iliyoachwa wazi na ACT ya Yule mama.

10. Kina Acacia watamwaga mihela kibao. Wajanja watazila.
 

pagalwema

Member
Sep 17, 2018
95
150
Wa ng'ambo ndio mwanacha asili
Na ana watu asili mwenye nguvu asili
Mnunuzi ameshasalim amli kutokana na mchaka mchaka wa siasa aliyecheza muvi Nairobi bado simzunguzii sana lakini ....
Kuhusu wabunge uliowataja ni wabunge Wa taifa hivyo wanajimbo wakijivuruga wametuvuruga na wengine
Sizani kama pengo La kafulila limezibika

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom