Kwetikavu HandeniNaomba uzi huu uwe natija kwa wote watakao itaji huduma kutoka kilingeni. Na wale ambao wataleta habari sijui za yesu, Mungu na wengine mara sijui nini, huu uzi sio wao maana hayajawakuta.
Naomba nimpe pasi honorable Dr Mshana Jr awezeku-share nasi vilinge mbali mbali anavyovifahamu kutoka katika kila kanda, mkoa, wilaya ya nchi bila kusahau jina na kijiji.
UPDATES KUTOKA MALEGENDARI
01. Kwansisi Handeni Tanga
02. Mapango ya Amboni Tanga
03. Majani mapana Tanga
04. Ludewa njombe vijiji vya Mundende, ibumi, ludende au nenda sehemu inaitwa JIWE LIGANGA
05. Kiwila, ngosi ziwani
06. Mwamboni Tanga
07. Vudee Same
08. Tukuyu Ushirika kijiji cha Utete ( nasikia mtaalam wa hapa ni tapeli)
09. Weruweru... Hai Kilimanjaro
10. Chitipa, mpakani mwa Ileje na Malawi na Zambia.
11. Mwandoya Bariadi - nasikia mpaka helicopters zikiwa na waheshimiwa uwa zinatua huku
12. Liwale, kuna kijiji kinaitwa Ngende.
13. simiyu Longa Lombogo
14. Kijiji cha Ikungulyabashashi kipo bariadi unashukia senta ya nyakabindi
15.Tanga mazinde kuna sehemu wanaita TORONTO ulizia mafundi.
Nitaendelea kuongeza kadili vilinge vinavyozidi kutambulishwa wachangiaji.
Na wewe unaefahamu machaka yanayotoa huduma zilizonyooka unakaribishwa pia kuchangia.
Mimi nimekaa pale nachukua notisi.
Kweli ni vizuri Kilinge kikawa specific kama ni Mtu anatahitaji kisasi cha kulipua Askari walioua ndugu kwenye maandamano ajue anaenda wapi.Mngekua mnasema na hivo vilinge ni vizuri kwenye nini....nsijeenda huko malawi kumbe kilinge cha pesa mie napeleka mapenzi mganga akaniona falah
Asante kwa updateKwetikavu Handeni
Uongo mchana kweupe...chai ya nazi.Nimezunguka vilinge vingi nimechanjwa chale nyingi sana,nimeoga dawa barabarani mchana,nimetambika mizimu,nimesomewa vitabu yasini ,nimevaa mabangili mapete,ushnga,nimecheza ngoma za mizimu.
nimechinja sana kuku,mbuzi ,kondoo
lakini yote haikusaidia.
nimepoteza pesa nyingi sana.
NILICHOJIFUNZA KWA WAGANGA WA KIENYEJI
1.wao ni binadamu kama sisi na wao pia wana matatizo yao kama sisi,na wao pia wanakufa kama sisi
wao hawana kama binadamu hawana nguvu ya ziada au uwezo wa ziada kama binadamu ISIPOKUWA wanategemea nguvu kutoka kwa MAJINI ,au MIZIMU ambayo ni majini ya ukoo..au kutoka KUZIMU kwa mapepo mashetani.
wao ni kiti wanakaliwa na mapepo majini/mamizimu majini ya ukoo..hayo majini ndiyo yanayowafundisha ushirikina uchawi na uganga wa kienyeji ..na mganga wa kienyeji na mchawi ni kitu kimoja ..na madhabahu yao ni moja na madhabahu ya kuzimu ya shetani na wachawi na mapepo na majini na mizimu.
hivyo mganga atapandisha mzimu wake ,au majini yake ,au walimu wake ,au wazee wake ,au wakuu wake..ROHO YA MAPEPO ndani yake itaongea kupitia kinywa chake ndio itakayofanya kazi ta ramli na ushirikina juu yako unaitwa uaguzi.
UKWELI NI KWAMBA
Pepo hawezi kumtoa pepo mwingine na kama akifanya hivyo ufalme wao wa giza umefitinika.
atamuita pepo aliyeko ndani yako alipuke atamoandisha ,akipanda hawezi kumtoa atamsihi aseme anataka aletewe nini ili atulie ,ila hawezi kutoka ,atatulia kwa muda,au atakuwekea mapepo mengine zaidi
pia anaweza kukuibia nyota yako,au kukuchukua msukule ,au kukuingiza katika uganga na uchawi ,au kukutoa kafara ,au kukuloga mana mganga wa kienyeji naye pia ni mchawi.
DAWA YA KWELI YA KUPONYA MATATIZO YOTE...ni YESU PEKE YAKE.
Hakuna dawa nyingine zaidi ya jina la Yesu..hakuna uponyaji mwingine zaidi ya jina la Yesu..damu ya Yesu.