Vileja vya njugu (peanut)

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,906
Mahitaji:

- Karanga robo zisage ziwe laini kiasi

- Mayai 5 tenganisha kiini na ute

- Custard 4 teaspoon
Baking powder 1/2 teaspoon

- Sukari 450g

- Hiliki 1/2 teaspoon

- Arki flavor upendayo

- Siagi 450g

- Unga vikombe 4 vya chai usijaze sana

Matayarisho:

- Saga sukari na siari hadi siagi iande kuwa light rangi

- Weka hiliki iliotangwa saga vizuri

- Weka viini vya mayai moja baada ya jengine huku unachanganya vizuri hadi mchanganyiko ulainike mimina na arki

- Chunga unga kwa chungio alafu changanya na baking powder na custard

- Changanya katika mchangiko wako taratibu hadi upate mchanganyiko mzito

- Tengeneza viduara vidogo vidogo kupitia huo mchanganyiko

- Pakaa ute wa yai juu yake (usiwe chini)

- Pakaa na njugu (peanut) juu yake

- Bake 350 moto hadi viwe light brown

- Toa acha kabisa vipoe

- Weka katika bakuli safi na hifadhi sehem nzuri


Nawatakia maandalizi mema ya eid����������

Nawapenda wote ������
 
Cc atoto Mrs Kharusy Angel Nylon Heaven on Earth Kim nana gorgeousmimi mwana ally ImageUploadedByJamiiForums1437035182.034896.jpg
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom