Carleen
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 8,407
- 28,837
Kwa mlioko Dar, Poleni kwa mgao wa kuanzia maji, umeme mpaka mapenzi, ila ndugu zangu tutafika kwa Baba tuko hoi sana maskiini, imagine duniani tunateseka hivii na bado huko naskia kuna moto tena..! Nyieeeeeeh'..!
Nisiwachoshe maana mshajichokea zenu tayari, kuna siku natoka zangu huko 'duniani' ilikuwa mida ya jioni ndiyo narudi zangu nyumbani, ile natoka getini nikakuta kuna watu wengi kweli wamekaa hapo pia wapo dereva toyo wamepaki kwa pembeni kidogo..!
Kama mnavyojua mdada ukipita mbele ya watu wengi ule ujasiri huwa unapotea tu ghafla, unatafuta cha kuzugia.! Luckily, nilikuwa niko na simu mkononi na kuna voice note ya whatsap nilikuwa nimetoka iskiza, ikabidi na mie nianze kurekodi V.N kujibu, shida hasa ilikuwa tu nivuke kwenye wale watu wengi, na venye walikuwa wananikodolea macho ndiyo nikahisi kuzimia kabisa.!
Sikupita hata hatua nyingi barabarani kwenyewe sijafika, nikaanza kuitwa na baadhi ya wale toyo 'swahiibaaa' 'swahibaaa', nikawaskia kiukweli ila nikajikausha mazima, nikaona enhee' washaanza uchokozi hawa bila shaka, maana akili zao huwa wanazijua wenyewe,
Nikaona wee' wasinizoee ndiyo kwanza nikazidi kuzidisha mashauzi na kutembea kwa pozi ili nijifanye niko serious na busy mradi tu waniache, pochi mkononi, maji yangu ya kunywa kisha nikakaza macho kwenye simu yangu nikajitia 'u-business face', dear Lord, laiti ningejua ningesimama niwaskize eti hata.! Lakini ile kiburi ya uzima itakuwa imeenda wapi sahiyo maskiini.!!
Nafika mbele kidogo, nikashangaa mbona kama hatua zangu hazizuiliwi na ile kimini tena nini kimetukia ghafla..!? Haha.! Sitaki kukumbuka ile siku walaqhi'..! Nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie huko.! Kumbe watu wote walivyokuwa wananishangaa na toyo wananiita waniambie ni namna zipu ya mini skirt kuna namna nilikuwa imeachia huko nyuma.!
So kadri natembea na yenyewe inazidi kushuka..! Jizoooozi..! Niliishiwa pozi, uso ulinishuka na yale mashauzi yakayeyuka yooote ghafla kama siagi motoni.! Nilijikuta naweka maji chini, pochi na simu bila kujijua wala kujali tena..! Nikakamata skirt yangu nikaibana zipu haraka haraka hapo najikaza nisianguke.! Ningechelewa ningeiokotea magotini.. Haha.! Nyieeeeh'..!
Niliinua vitu vyangu ardhini bila kugeuza hata shingo kwa aibu, nikajikuta napanda daladala niliyokutana nayo ya kwanza ambayo hata haina uelekeo ninaoenda shida yangu tu ni kuondoka lile eneo, catwalk ikapotea ghafla ikawa ni mwendo wa kuruta, nimekaa kwenye daladala nikawa nahisi kama kila mtu anajua kilichotokea.!!
Ila tbh, nilijifunza kitu kikubwa sana siku ile,
anyways, nimejikuta tu nashea.!! Uliwahi aibika mbele za watu.? Ilikuwaje.?

machali walibaki kumwambia papuchi yako inaonesha tamu. Baadhi ya wanawake wakiitwa akili zao wanaona wanataka kupewa mtongozo tu.