Vikwazo vya mradi wa bomba kutoka Hoima mpaka Lamu

kimwela

Member
Mar 25, 2016
17
25
Taasisi ya Utafiti ya BMI iliyopewa kandarasi ya kufanya utafiti wa vikwazo vya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi linalotarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 1500 sawa na maili 930 kutoka katika visima vya mafuta vilivyoko huko Kaiso Tonya Magharibi mwa mji wa Hoima nchini Uganda hadi katika mji wa bandari wa Lamu nchini Kenya unakabiliwa na vikwazo kadhaa.
  • Kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kumewafanya wawekezaji katika mradi huo kurudi nyuma kutokana na kupanda kwa gharama za mradi huo, pia kumeifanya Serikali ya Uganda kujipanga upya kuongeza kiwango cha fedha ili kuutekeleza mradi huo na kupunguza nakisi ya bajeti,
  • Mafuta yatakayosafirishwa na bomba hilo yana tabia ya "waxy" hivyo kuhitaji nuru joto la kutosha ndani ya bomba ili kuhifadhi ubora wa mafuta hayo. Changamoto iliyopo ni namna ya kupata technolojia yenye gharama nanuu ili mradi huo ukamilike,
  • Jiografia ya eneo ambalo ujenzi wa bomba hilo utapita ni katika maeneo yaliyo chepechepe (swamp areas), hali hiyo nayo yaweza kuwa ni kikwazo kimojawapo cha kukamilisha mradi huo kwa wakati,
  • Njia inayopendekezwa na Serikali ya Kenya kupitisha mradi huo [ambao kama utatekelezwa utakuwa maradi mrefu zaidi wa ujenzi wa bomba la mafuta katika bara la Afrika] utapita katika mbuga za wanyama na hifadhi za taifa, ukiruhusiwa kuendelea utahatarisha maisha na malisho ya wanyama na kuharibu ushoroba wa Kaskazinimagharibi mwa kenya,
  • Kitisho kikubwa kinachokabili ujenzi wa mradi wa bomba hilo ni ukosefu wa usalama huko Kaskazini mwa Kenya ambako waasi wa Alshababu wamekuwa ni kitisho kikubwa kwa ujenzi wa mradi huo wenye gharama kubwa, [$bilioni nne za USA],
  • Changamoto ya ukosefu wa umeme wa uhakika nchini kenya kutafanya mradi huo kutokamilika kwa wakati hadi mwaka 2020,
  • Kukosekana kwa wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu katika tasnia ya ujenzi wa bomba hilo kutalazimu kuajiri wafanyakazi wengi wa kigeni, hilo litaongeza gharama za ujenzi wa mradi huo,
  • Tatizo jingine litakalo kwamisha mradi huo ni barabara mbovu zisizo faa kupitisha vifaa/mitambo na huduma kutoka bandari ya Mombasa hadi maeneo ya ndani ya Uganda kuelekea huko Hoima (Magharibi mwa Uganda), changamoto iliyopo ni kuwepo kwa milima na mabonde mengi upande wa Kenya,
  • Sababu nyingine inayotolewa na BMI ni ukosefu wa maelewano baina ya Kenya na Uganda kwamba nani atagharamia nini katika ujenzi wa mradi huo na taratibu za bima (insurance policy) zitahudumiwa kwa uwiano gani?, benki ya dunia ipo tayari kugharamia Kshs. 54 milioni tu,
  • Mpango wa Kenya ni kuunganisha ujenzi wa bomba la Hoima na visima vya mafuta vya bonde la Lokichar huko Kaskazini Magharibi mwa Kenya na bomba la mafuta kutoka jimbo la Unit Nchini Sudani kama njia mbadala ya bandari ya Sudani, na kuifanya Kenya kuwa kiungo muhimu cha biashara hiyo, kunaifanya Kenya kupigania mradi huo kufa na kupona.
 
Aisee vikwazo vingi sana, walete tu Tanzania huo mradi maana hakuna namna nyingine
 
Tanzania kwanza Tanga kivutio kwa mradi huo mkubwa manyang'au watatuita Giants uuhuuuuu kule Kenya mradi haufai kwenda kabisa si wamewachokoza njaa kali nywele zilizorambwa na mbwa nao kumbe ni wakali, your Enemie's Weakness it is an Opportunities for sisi uhuuuuuu
 
Bado kulipia radhi
Utambue kuwa radhi ya Kenya ipo mikononi mwa Watu wenye mipesa yao

Kwahio fidia itakuwa kibwa
 
Duuuh hvi kwani bado tamko lijatoka kwamba mzigo utaelekea wap? mbna porojo haziish?
 
Kenya walishapotez huu mradi, nina wasi wasi kama kenya wamegundua mafuta. Kenya hawana mafuta wanataka kuiba ya Uganda.
Kama wanayo ni kiasi gani kilichogunduliwa? Na kama wana ya kwao kwa nini wapiganie kufa na kupona bomba ya uganda?
 
Kenya wamegundua mafuta katika bonde la ufa Turkana, lakini kiwango chake ni kidogo ukilinganisha na ugunduzi wa Uganda. Wenzetu wakenya ni watu wa fursa, kama watafanikiwa kuishawishi Juba ipitishe bomba lake Kenya hadi Mombasa itakuwa fursa nzuri kwao kuimarika kiuchumi na kisiasa.
 
Back
Top Bottom